UTAWALA MKUU

UONGOZI WA JATU PLC

WASIFU WA WAJUMBE WA BODI YA JATU PLC

MWENYEKITI WA BODI YA JATU PLC

MHANDISI. DOKTA. ZAIPUNA O. YONAH

Ni mtanzania mwenye umri wa miaka (59), ana shahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme toka chuo kikuu cha Dar es Salaam (1985), Shahada ya Uzamili (1988) na ya Uzamivu (1994) toka Chuo Kikuu cha Saskatchewan, Canada. Ni Mhandisi Mshauri katika taaluma ya Mawasiliano na Tehama aliyesajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania.Dr Yonah ni Mkufunzi Mwandamizi mwenye ushirikiano na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela -Arusha Tanzania na Kampuni ya Applied Engineering & ByteWorks (T) Ltd. (2013 – hadi leo). Aidha amewahi kufundisha Chuo Kikuu cha DSM (1985-2000), kuwa Mkurugenzi wa Mitandao na Bidhaa za Tehama TTCL (1998 – 2008). Alikuwa Mkurugenzi wa Tehama Kitaifa katika iliokuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakati ambapo alisimamia ubunifu, usanifu na utekelezaji wa Mradi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (2008 – 2013). Mhandisi Dr Yonah analeta JATU uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi, usimamizi, kutafiti, kubuni, kusanifu, kutekeleza na kuendesha mitambo ya umeme na mitandao mikubwa ya mawasiliano na mifumo ya Tehama ya kutoa huduma na kuendesha biashara.

MKURUGENZI MTENDAJI

peter isare gasaya

PETER ISARE (1990) (Tanzanian) Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa JATU PLC. Anamiliki Digrii ya sheria (Hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Isare ana malengo makubwa, shupavu na mjasiriamali mwenye ujuzi, anaamini mabadiliko ya kiuchumi ndo mbinu za kuwaokoa maskini, kabla ya kuanzisha JATU alianzisha shirika lisilo la faida (2015) lililoitwa ulinzi wa kisheria na shirika la kuboresha maisha ili kukabiliana na uharibifu wa umaskini na ulinzi wa haki za binadamu. Amehudhuria mafunzo na semina katika uongozi, ujasiriamali na makampuni kadhaa.

katibu wa bodi

MOHAMED ISSA SIMBANO

Mohamed Issa Simbano ni kongozi mwenye shauku na rekodi ya muda mrefu ya usimamizi wa mafanikio, ISSA ana ujuzi kwenye sekta ya sheria, masuala ya uchumi, kijamii na uongozi. Amekuwa katika sekta ya utawala kwa zaidi ya miaka 5. Yeye ni kiongozi mwenye kuchochea maendeleo na hamasa kuboresha ufanisi kwenye kazi. Pia ana maono ya mbele kwenye kujenga na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa kampuni. Anaweza kushinikiza uboreshaji wa utendaji wakati huo huo chachu ya ukuaji kitaaluma kazini. Daima huhakikisha kuwa malengo ya wazi na matarajio yanayotolewa na kukamilika kwa wakati.

WASIFU WA WATUMISHI WA JATU

msimamizi MKUU wa fedha

esther MARINO CHRISTIAN

Esther Marino ni mmiliki wa shahada ya Mabenki na Fedha kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) 2012-2015. Esther ni Mhasibu Mkuu wa JATU PLC kwa miaka miwili sasa. Pia ana uzoefu mkubwa katika Hesabu na Fedha amefanya kazi kama mwanafunzi(trainee) katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

mkuu idara ya rasilimali watu

ESTHER PHILEMON KIUYA

Esther Philemon ni mhitimu katika Sayansi ya Jamii na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (2012 – 2015). Esther Philemon ni kiongozi mwenye ujuzi na taaluma katika sekta ya  rasilimali watu kwa zaidi ya miaka 3. Kabla ya kujiunga na JATU, alifanya kazi kama katibu wa LPLIO.

MKUU WA IDARA YA TEHAMA

MOSES LUKOO WILLIAM

MOSES alikamilisha masomo yake ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) katika Chuo cha Biashara na Usimamizi cha St. Joseph, Morogoro Tanzania. Baada ya kumaliza masomo yake, alitunzwa na uongozi wa chuo na usimamizi kama mwanafunzi bora katika masomo ya mwaka 2015/2016. Ana miaka mitatu ya uzoefu wa kazi na taaluma kubwa katika kusimamia mifumo ya Tehama. Ni kijana mbobezi na mjuzi wa Mifumo ya Usimamizi, Ufumbuzi wa Mitandao, Matengenezo na ukarabati wa vifaa vya kompyuta, Graphics Design na masuala ya multimedia. Lakini pia, kabla ya kujiunga na JATU amekuwa akifanya kazi katika maeneo mbalimbali ya ICT akifanya kazi na mashirika mbalimbali kama mtaalamu wa ICT na mshauri.

MKUU WA IDARA YA MASOKO

MARRY RICHARD CHULE

Mary Richard Chulle ni mtumishi mwenye sifa ya uzoefu wa Masoko na Mahusiano ya Umma, alipata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine mwaka 2015, ambako alisomea shahada katika Masoko na Uhusiano wa Umma. Ana uzoefu wa miaka zaidi ya minne(4) katika fani hiyo. Mary sasa anafanya kazi Jatu kama Mkuu wa idara ya  Masoko. Pia alifanya kazi kampuni kama Sunda International kama mtoa huduma kwa wateja na afisa wa mauzo (2017-2018), kama karani wa data katika kampuni ya Marie Stopes Tanzania (2016-2017). Afisa wa Mradi katika Maendeleo ya Jamii ya Kifaru Community Development (2014-2016) na Afisa wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa Wilaya ya Kibaha (2014).