MILIKI HISA ZA JATU

Je unahitaji kumiliki hisa za JATU?

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni, ambapo mwanachama atakaponunua hisa za JATU PLC atakua amechangia ama kuongeza mtaji katika kampuni na hivyo kuiwezesha kampuni kuzidi kukua zaidi kwa kubuni miradi mikubwa na endelevu.

Zifuatazo ni faida za kumiliki hisa za JATU

  • Kuweza kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya JATU PLC,kama kilimo,viwanda,masoko na mikopo.
  • Kupata gawio la faida kila mwisho wa mwaka.
  • Kumiliki cheti cha hisa ambacho kitakuwezesha kupata mikopo katika taasisi za kifedha.
  • Kuwa mwanachama mnufaika wa JATU SACCOS.
  • Usalama,kununua hisa katika kampuni iliyoorodheshwa katika soko la hisa kuna uhakika wa usalama wa fedha yako kwasababu kampuni zinasimamiwa chini ya vyombo vya serikali kama BRELA, CMSA na DSE hivyo kumuhakikishia muwekezaji usalama wa fedha zake.