MWANACHAMA MWANAHISA

Bofya link hii kujiunga https://jatu.co.tz/admin/sw/self_registration

Huyu ni mwanachama anayejiunga kwa kulipia shilingi 5,000/= na badae akanunua hisa za kampuni kuanzia angalau hisa 50. Hisa moja ya Jatu inauzwa …(bei itatangazwa baadae). Mwanachama huyu atapata faida zifuatazo akiwa mwanahisa gawio la kila mwaka kutokana na hisa zake, kushiriki katika miradi ya JATU, kupata mkopo wa kilimo usiokua na riba kupitia JATU SACCOS, kumiliki cheti cha hisa ambacho kinaweza kutumika kama dhamana katika taasisi mbalimbali za kifedha

Vigezo na Mashart kwa yeyote anayetaka kujiunga Jatu:

Kabla hujajiunga na jatu hakikisha umeifahamu vyema kampuni hii na kwamba unajiunga kwa hiari yako wewe mwenyewe, pia hakikisha una namba ya mdhamini Yaani mtu ambaye tayari ni mwanachama wa Jatu na pia hakikisha unayo namba ya wakala wa Jatu, namba hizi ni lazima uwenazo na uzijaze kwenye fomu yako ili upate usajili, mdhamini wako ni mtu aliyekupa habari kuhusu jatu na wakala ni mwakilishi wa kampuni ambaye ni msimamizi wa mafunzo yako ambaye pia atahakikisha unapata huduma zote za jatu kwa urahisi. Namba ya wakala inapatikana kutoka kwa mdhamini wako. Vipengele muhimu ambavyo unapaswa kujua kuhusu jatu ni pamoja na;

  • Jatu ni kampuni ya Umma inayojihusisha na kilimo, viwanda, masoko na mikopo. Inawaunganisha wakulima na kuwawezesha mikopo ya pembejeo bila riba na kisha hununua mazao hayo na kuandaa bidhaa ambazo zinauzwa kwa wanachama kwa mfumo wa masoko ya mtandao (networking).
  • Kampuni inamilikiwa na Umma kwa maana ya kwamba mtu yeyote anaruhusiwa kununua hisa za Jatu PLC, kampuni tayari imeshasajiriwa DSE ambapo vipande takribani milion 15 viliwekwa sokoni yaani INITIAL PUBLIC OFFER (IPO) na hisa zake zitaanza kupatikana rasmi muda mfupi tu katika soko la hisa DSE ambapo hapo sasa mwanachama atanunua hisa kutokana na bei ya soko.
  • Mwanachama wa jatu anayejiunga kwa shilingi elfu tano na mara baada ya hapo mwanachama Mteja anaweza kufanya manunuzi na kuunganisha wanachama wengine ili kujitengenezea gawio kubwa kila mwisho wa mwezi kutokana na manunuzi yake binafsi au manunuzi ya timu yake.
  • Kila mwanachama anayejiunga atalazimika kulipia gharama za uendeshwaji wa akaunti mara tu baada ya kujiunga kama ada ambapo baada ya hapo hatokatwa tena na ataendelea kulipwa kila mwisho wa mwezi kutokana na manunuzi yake na ya mtandao wake.
  • Kupitia Mfumo huu unaweza kuwa balozi wa Jatu ambapo kama una bidhaa zako utaziuza kupitia mfumo wa Jatu bila kulipia ada yoyote ile na utafaidika kutokana na ubunifu wako. Walengwa hapa ni wazalishaji wote wa bidhaa za chakula na usafi, kama unazo bidhaa kama hizo na hauna soko la uhakika sasa unaweza kuzisajili katika mfumo wa jatu na ukawa na soko la uhakika kitaifa na kimataifa.
  • Kampuni ya Jatu kupitia saccos yake inawawezesha wanachama wake kupata bima ya afya kwa gharama nafuu, ili kupata huduma hii ni lazima ujiunge na Jatu Saccos Ltd.
  • Ukinunua hisa za kampuni ya Jatu, hisa moja kwa sasa ni tshs. ….(bei itatangazwa baadae) kiwango cha chini kununua ni angalau hisa 50, lakini pia unaweza kujaza fomu ya ahadi ya kununua hisa na ukawa unalipia kidogo kidogo wakati kampuni inajiandaa kuorodhesha hisa zake katika soko la hisa.
  • Kampuni hii imedhamiria kuwafikia watanzania wote, wa mjini na vijijini, wakulima na wateja wa bidhaa na mazao ya kilimo, wajasiliamali wote wanao hitaji masoko ya uhakika, wakulima wanaohitaji pembejeo na elimu ya kilimo pamoja na wawekezaji wanao hitaji kununua hisa na kuwekeza na Jatu.
  • Tafadhali tambua kwamba kama umejiunga Jatu PLC na ukiwa hautumii bidhaa za Jatu au kujenga mtandao unao nunua bidhaa zilizo katika mfumo wetu; hutopata gawio lolote lile la mwezi, na kama gawio lako halijafika shilingi Elfu tatu (3000) kila mwezi hutaweza pia kulipwa, yaani tunalipa kuanzia Tsh. 3000/= na kuendelea kila mwezi na ukishalipwa akaunti yako inaanza upya, hivyo hivyo ukishindwa kufikisha 3000/= kiasi kilichopo kwenye akaunti yako kitaingizwa kwenye kampuni na hivyo mwezi unaofuata utaanza upya.
  • Mtu yeyote atakayefungua akaunti katika mfumo wa JATU na akamaliza mwezi mzima bila aidha kununua bidhaa au kuunga mwanachama mpya, tutamfuta kutoka kwenye orodha ya wanachama wa JATU na namba yake atapewa mtu mwingine aliyetayari kujiunga na kujenga mtandao wa wateja.

Kwa kuwa umesoma maelezo yetu yote kuanzia namba 1-10, ni Imani yetu kwamba umetuelewa na ndo maana umeamua kutengeneza akaunti yako katika mfumo wa Jatu PLC, hivyo basi kanuni na taratibu za Jatu PLC zitatumika kukuongoza na ni wajibu wako kuziheshimu na kuzifuata.