MWANACHAMA MTEJA

Bofya link hii kujiunga kama Mwanachama mteja https://jatu.co.tz/admin/sw/self_registration

Huyu ni mtu yeyote anayejiunga na kampuni kwa lengo la kununua bidhaa za Jatu. Mwanachama huyu analipia kiingilio cha shilingi 5,000/= na kujaza fomu ya uanachama. Mwanachama huyu anahaki ya kutengeneza mtandao na akapata malipo ya kila mwezi kutokana na manunuzi yake na ya wanamtandao wake. Mwanachama huyu anaruhusiwa kushiriki miradi mingine ya kampuni kama vile kilimo, saccos, masoko au kununua hisa za Jatu.

Vigezo na Masharti kwa anayetaka kujiunga Jatu Plc:

Kabla hujajiunga na Jatu hakikisha umeifahamu vyema kampuni hii na kwamba unajiunga kwa hiari yako wewe mwenyewe, pia hakikisha una namba ya mdhamini yaani mtu ambaye tayari ni mwanachama wa Jatu na pia hakikisha unayo namba ya wakala wa Jatu, namba hizi ni lazima uwenazo na uzijaze kwenye fomu yako ili upate usajili, mdhamini wako ni mtu aliyekupa habari kuhusu Jatu na wakala ni mwakilishi wa kampuni ambaye ni msimamizi wa mafunzo yako ambaye pia atahakikisha unapata huduma zote za Jatu kwa urahisi. Namba ya wakala inapatikana kutoka kwa mdhamini wako. Vipengele muhimu ambavyo unapaswa kujua kuhusu Jatu ni pamoja na;

  • Jatu ni kampuni ya umma inayojihusisha na kilimo, viwanda, masoko na mikopo. Inawaunganisha wakulima na kuwawezesha mikopo ya pembejeo bila riba na kisha hununua mazao hayo na kuandaa bidhaa ambazo zinauzwa kwa wanachama kwa mfumo wa masoko ya mtandao (network marketing).
  • Kampuni inamilikiwa na umma kwa maana ya kwamba mtu yeyote anaruhusiwa kununua hisa za Jatu PLC, kampuni imeshasajiliwa katika soko la hisa, na unaruhusiwa kununua hisa kwa kadri utakavyoweza kupitia brokers mbalimbali ama tupigie 0758 495 271 kwa msaada zaidi kuhusu masuala ya hisa.
  • Kupitia Mfumo huu unaweza kuwa balozi wa Jatu ambapo kama una bidhaa zako utaziuza kupitia mfumo wetu (JATU MARKET) bila kulipia ada yoyote ile na utafaidika kutokana na ubunifu wako. Walengwa hapa ni wazalishaji wote wa bidhaa za chakula na usafi, kama unazo bidhaa kama hizo na hauna soko la uhakika sasa unaweza kuzisajili katika mfumo wa Jatu Market na ukawa na soko la uhakika kitaifa na kimataifa.
  • Kampuni ya Jatu kupitia saccos yake inawawezesha wanachama wake kupata bima ya afya kwa gharama nafuu, ili kupata huduma hii ni lazima ujiunge na Jatu Saccos Ltd.
  • Ili kushiriki kilimo ndani ya Jatu ni lazima ununue hisa za Jatu ambazo zinapatikana soko la hisa DSE kupitia brokers mbalimbali lakini pia unaweza kununua hisa kwa kupitia simu janja yako.Ambapo kama unataka kulima kuanzia ekari moja mpaka ekari 49, utalima kwa uwiano wa 1:50 yaani hisa 50 kwa kila ekari, na kwa wale wanaotaka kari 50 na kuendelea watalima kwa uwiano wa 1:500 yaani hisa 500 kwa kila ekari.
  • Kampuni hii imedhamiria kuwafikia watanzania wote, wa mjini na vijijini, wakulima na wateja wa bidhaa na mazao ya kilimo, wajasiriamali wote wanaohitaji masoko ya uhakika, wakulima wanaohitaji pembejeo na elimu ya kilimo pamoja na wawekezaji wanaohitaji kununua hisa na kuwekeza na Jatu Plc
  • Tafadhali tambua kwamba kama umejiunga Jatu PLC na ukiwa hautumii bidhaa za Jatu au kujenga mtandao unao nunua bidhaa zilizo katika mfumo wetu; hutopata gawio lolote lile la mwezi, na kama gawio lako halijafika shilingi Elfu tatu (3000) kila mwezi hutaweza pia kulipwa, yaani tunalipa kuanzia Tsh. 3000/= na kuendelea kila mwezi na ukishalipwa akaunti yako inaanza upya, hivyo hivyo ukishindwa kufikisha 3000/= kiasi kilichopo kwenye akaunti yako kitaingizwa kwenye kampuni na hivyo mwezi unaofuata utaanza upya.

Kwa kuwa umesoma maelezo yetu yote kuanzia namba 1-7, ni Imani yetu kwamba umetuelewa na ndio maana umeamua kutengeneza akaunti yako katika mfumo wa Jatu Plc, hivyo basi kanuni na taratibu za Jatu Plc zitatumika kukuongoza na ni wajibu wako kuziheshimu na kuzifuata.