MTANZANIA MZALENDO

Bofya link hii kujiunga https://jatu.co.tz/admin/sw/self_registration

JINSI YA KUJIUNGA NA JATU KWA WATANZANIA WALIO NJE YA TANZANIA

  1. Ingia katika website au Application (app) ya Jatu, jina la website yetu ni http://jatu.co.tz na App yetu ni JATU MARKET ukiingia Playstore au Appstore una search neno JATU MARKET utaiona.
  2. Katika App ya JATU Ukishapakua utaona sehemu ya kujaza namba ya uanachama na neno la siri hapo ni kwa mwanachama aliyewahi kujiunga. Kwa mwanachama ambae ni kwa mara ya kwanza nenda SEHEMU YA CHINI kuna neno sina akaunti tengeneza mpya na utalipia shilingi elfu elfu tano kama kiingilio lakini pia kwa ajili ya kuboresha akaunti yako.
  3. Utajaza taarifa zako zote hapo ikiwa ni majina kamili na taarifa zingine namba ya mdhamini tumia ya mtu ambaye alikupa link (habari) ya jatu kwa mara kwanza(wasiliana nae atakupa namba yake ya Jatu ndo inatumika kama sponsor). Kuhusu namba ya wakala unaweza kumuuliza huyo atakaye kupa sponsor namba au kama zote hizo huna wasiliana nasi kupitia namba 0758396767 kwa msaada zaidi.
  4. Ukikamilisha usajili wako basi hapo utasubiria upewe namba ya uanachama na neno la siri ambapo utawasiliana na namba hii ambayo ni ya huduma kwa wateja kutoka Makao Makuu Dar es salaam, Tanzania. (Mtumie ujumbe Whatsap atakujibu mara moja na atakutumia namba yako kwani ingeweza kuja moja kwa moja lakini bado mfumo wetu haujaweza kuhudumia watu walio nje ya Tanzania moja kwa moja)
  5. Baada ya hapo utakuwa mwanachama na unaweza kuendelea kujiunga na fursa mbalimbali zilipo Jatu kama vile kununua mashamba au kukodi kupitia hiyo mfumo huo na taarifa zote zitakuwa zinaonekana kupitia simu yako au komputer yako.

Angalizo:
Katika kujaza fomu yako ya uanachama taarifa zako za makazi tunaomba ujaze taarifa za hapa Tanzania kwa maana ya mkoa, wilaya na Kata ulipozaliwa ~ hizi zitakuja moja kwa moja kazi yako itakuwa ni kuchagua tu, mfano ukichagua mkoa wa Arusha utaletewa pia wilaya ukichagua wilaya utaletewa kata/Tarafa. Na baada ya hapo kwenye sehemu ya Mtaa tunaomba uandike jina la nchi na address ya eneo ambalo kwa sasa unaishi mfano; USA, Texas area 10 ….nk

JATU~ JENGA AFYA, TOKOMEZA UMASIKINI