MASWALI NA MAJIBU

Najiunga vipi na JATU na Kiwango cha chini cha kununua hisa ni kipi?

Kujiunga tafadhali ingia playstore pakua App yetu na uweze kujiunga Kupitia App ya Jatu au kama yupo karibu na ofisi zetu basi wafike ofisini moja kwa moja ili kuweza kujifunza zaidi (Sabasaba Maonesho -Dar Es salaam, Makao Makuu Posta PPF House Ghorofa Na. 06) au karibu na branch zetu zilipo mikoani kama vile Arusha, Morogoro, Dodoma, Kiteto Manyara, Mtwara, Mwanza.
Kiwango cha chini cha kununua hisa kwa ajili ya kulima na JATU ni hisa 50

Ikiwa nimejiunga na JATU PLC, itanisaidiaje?

Ikiwa umejiunga na JATU, itakusaidia katika mambo yafuatayo;

• Itakusaidia kumiliki shamba lako la kisasa uweze kushiriki kilimo cha faida

• Itakupatia wataalamu ambao watasimamia mashamba yetu jumuishi

• Itakusaidia kupata soko kwa kununua mazao yako yote uliyovuna

• Itakusaidia kukupatia mkopo wa kilimo ambao hauna riba pia mkopo wa maendeleo wenye riba

nafuu

Kwanini JATU PLC inapeleka hisa sokoni DSE?

JATU PLC ni kampuni pekee Tanzania inayojishughulisha na kilimo inayoingia katika soko la hisa DSE, na hii ni kwa sababu zifuatazo;

• Kununua mitambo pamoja na uchimbaji wa visima kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji

• Kununua zana za kisasa za kilimo

• Kununua ardhi kwa ajili ya utanuzi wa mashamba

• Kujenga viwanda vya kuchakata nafaka katika kuongeza thamani ya mazao Kuboresha miundombinu ya utendaji katika kampuni ikiwemo idara ya miko

Kwanini niwekeze JATU PLC?

• Kuweza kushiriki katika miradi ya kilimo cha kisasa ya JATU

• Kunufaika na mikopo isio na riba ya kilimo

• Kunufaika na gawio la kila mwezi kutokana na manunuzi yako ya bidhaa za JATU

• Kunufaika na gawio la faida la kila mwaka

• Kunufaika na Bima ya Afya

Mashamba ya JATU yanapatikana katika mikoa gani?

Kwa sasa JATU ina mashamba katika mikoa ifuatayo:

• Manyara – Kiteto

• Tanga – Kilindi, Handeni

• Morogoro – Kilombero

  • Njombe – Taweta
  • Rukwa – Sumbawanga

JATU imejikita katika kilimo cha mazao yapi?

Kwa sasa JATU imejikita katika kilimo cha maharage na machungwa huko Kilindi,handeni-Tanga, mpunga huko Kilombero-Morogoro, mahindi na alizeti huko Kiteto-Manyara na parachichi huko taweta Njombe

Je, nikiwa na shamba langu binafsi JATU itanisaidiaje?

Ukiwa una shamba lako binafsi JATU itakuwezesha kwa kukupa mkopo wa maendeleo wenye riba nafuu kabisa.

Wengine sio member wa Sacos wala mwanakikundi wa JATU na pia kama unavyoona hizo ghalama za kujiunga na vigezo ni vingi how can you help him In fact anaitaji kuanza  shughuli za kilimo na mtaji wake unakizi kwnye  kukodisha shamba tu na kama atalipia ghalama nyingine atashindwa kufanya shughuli za uzalishaji na lengo la JATU ni kumsaidia MTU.

Hapana ili uweze kushiriki kwenye kilimo inabid uwe na hisa angalau 50 kwa suala la mtaji ndo maana tunayo Saccos tunakopesha mkulima bila riba kwa mfano hapo kwenye hizo gharama za kilimo cha mahindi mkulima angepaswa awe na laki tisa 900,000 ili aweze kulima ekari moja lakini sasa kupitia jatu mkulima anahitaji tu kuwa n angalau laki 3 na ataweza kulima kisasa na kutengeneza faida kubwa

Je JATU inamsaidia mtu kupata shamba zuri lenye ubora na vigezo vinavyowezesha mtu kupata mazao bora ili kulipa mkopo huo?

Ndio na ndo maana tumetoa mchanganuo mapema ili tujiandae kwa kutafuta mashamba mazuri ili kuhakikishia kilimo chenye tija

Vipi JATU inaweka makisio ya mavuno kutegemea na Hali ya hewa,,wakati tunategemea kilimo kinachoendeshwa ni kilimo Cha kisasa ?

Tunafanya kilimo cha kisasa kabisa kwa kutumia wataalamu na vifaa vya kisasa hapo kitu pekee kilichopungua ni Umwagiliaji ambapo tayari tumeanza mchakato kwenye mashamba yetu ya Kiteto na tunaimani muda si mrefu mashamba yote ya Jatu yatakua chini ya umwagiliaji.

Je JATU ilianzishwa lini?

JATU PLC ilianzishwa mwaka 2016

Na je kama unashamba eneo lingine tofauti nahayo ulioyataja je JATU wanaweza kukusaidije?

Hapana kwa sasa tumejikita katika kilimo jumuishi cha pamoja kwani kinapunguza gharama na usumbufu katika usimamizi, lakini tutakupa mkopo binafsi wenye riba nafuu kukusaidia kufanikisha lengo lako

Namna ya kujiunga JATU Saccos inakuaje?

Kwanza lazima ujiunge JATU na uwe na hisa angalau 50. Baada ya hapo utajiunga JATU Saccos kwa kiingilio cha Tshs 10,000/-

Yaaan unafanya kilimo cha kisasa na unategemea mvua??? Kila siku wakulima kilio chao ni mvua sasa unatofauti gani na mkulima wa kawaida ikitokea mvua ikawa kinyume na mitazamo yenu?

Tunayo bima. Lakini pia tunao mradi wa Umwagiliaji kama unapenda kushiriki unashauriwa kununua kabisa shamba lako la kudumu then tuweke miundombinu ili uwe unalima kwa uhakika kila mara unapohitaji kufanya hivo ekari moja inauzwa 750,000/-

Mimi Nina swali nikilima na JATU naweza vuna mazao yangu nikaenda kuuza popote ?

Kwanza inabidi ufahamu soko la kwanza ni JATU kupitia viwanda vyake hivyo hatukushauri kuuza nje maana hata huko wananunua kwa bei sawa na yetu yaani bei ya sokoni iliopangwa na serikali

Najaribu kuona kwenye bei za kuvuna naona kama bado hatujafanya study ya kutosha. Bei za JATU zipo juu

Ni bei za kawaida sana. Usiangalie hiyo jumla ya gunia 30, angalia kwa gunia mkuu. Na hapo ni hadi store kabisa huingii tena gharama nyingine kama ilivyo kwa wakulima wengine wataingia gharama za kupeleka tena sokoni au kutunza ghalani

Mimi kama sitaki kilimi nataka Saccos tu najiungaje ili niwe mwanachama wa Saccos tu

Unaruhusiwa. Jiunge JATU nunua hisa then anza kuweka akiba Saccos utakopa

Hebu tupe jumla ni SHS ngapi Hadi niwe member, then Hadi niwe na eka 2, then Hadi ghalani. Na hapo sijui mteja anapatikana???

Mteja ni Jatu, so kuhusu soko ondoa wasiwasi kabisa

1. Kujiunga jatu free

2. Hisa 50= 125,000/-

3. Kujiunga Saccos = 10,000/-

4. Kukodi ekar 2 = 100,000/-

5. Akiba ya eka 2 = 514,000/-

Jumla kuu: 749,000/-

Kujiunga JATU free? Elfu 30 ni ya nini niliiona huko juu

Ukisoma fomu yetu inasema unaweza kulipia au ukajisajili free then utakua unakatwa taratibu kutokana na gawio unalopata kila mwezi kwa kununua bidhaa za jatu kupitia app ya jatu. So kuna option 2

Ndio natakiwa nije office kwa ajili ya kujiunga au nafanyaje ?

Unaweza tembelea ofisi ya karibu na mkoa uliopo au kujiunga online kupitia kwenye app yetu ya JATU nenda playstore andika JATU halafu download na jisajiri utaweza fanya manunuzi

Ikitokea mavuno hakuna nini kinatokea kwa wanachama ambao tumewekeza mitaji yetu.

Kuna bima ambayo inakuwezesha kurudisha gharama zako zote

Alafu watu wanapokuja na ideas hua hawasemi changamoto zaid ya mafanikio je hii project yenu ina changamoto zipi????

Changamoto kubwa ni hali ya hewa mkuu. Lakini tayari tumeanza kuijibu kwa kuanzisha miradi ya Umwagiliaji tunaamini baada ya awamu ya mazao haya mwakani tutalima kwa Umwagiliaji

Najaribu kuuliza basing kwenye kauli yako kuwa tunalima kisasa na tunamhakikishia mkulima mavuno kuanzia 30-40 gunia. So nauliza ikiwa chini ya hapo? Mnamlipa mkulima?

Hatuwezi kukulipa gunia 30 wakati tumevuna gunia 40 utatakiwa kulipwa gunia 40 lakini pia hatuwezi kukulipa gunia 40 wakati tumevuna gunia 10. Kumbuka sisi hatufanyi biashara ya kulima, tunachofanya tunakusaidia wewe ulime kitaalamu ili tununue mazao, kwa hiyo hatuna sababu ya kukulipa pasipo na uhalisia wa mazao

Nawezaje kupata taarifa zenu zaidi?

Tunapatikana pia kupitia kwenye website yetu http://www.jatu.co.tz au tufuatilie kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram na youtube andika jatu_plc au tutembelee kwenye ofisi zetu zilizopo mikoa karibia 7

Mnaposema kilimo cha umwagiliaji mna maana kuwa popote pale mtakapo ninunulia eneo nitapata uhakika wa maji kwa ajili ya shughuli ya umwagiliaji au mnanichimbia kisima sijaelewa wapi?

Kwenye mashamba yaliyonunuliwa tunafunga miundo mbinu ya umwagiliaji kwa kushirikiana na mkulima utachangia gharama kidogo ili mitambo iwezwe kufunga ulime kisasa bila kutegemea mvua

Ok, na je mnajihusisha na kilimo cha mbogamboga?

Hapana, kwa sasa tumejikita katika Mahindi, alizeti, maharage na Mpunga

Je kama ntalima shamba na JATU huko nami naishi Mkoa mwingine tena mbali na huko nilikolima, je usimamizi wake apo na JATU utakuwaje?

JATU anasimamia usimamizi wa shamba lako kwa uaminifu na weledi kabisa ndo maana umeona hapo kuna gharama ya usimamizi kwa hiyo usiwe shaka na hivi kuhusu umbali hata ukipata siku moja tu ukatembelea shamba inatosha

Naomba ufafanue hii ya bima ikoje?

Unapochukua mkopo kwa ajili ya kilimo JATU tunajua kuna changamoto nyingi ambazo zinaweza kupelekea hasara. Hizo changamoto tumetengeneza mfumo ambao utakuwezesha kurecover gharama zako (mtaji) wakati wa hasara ili uweze kuendelea na uwekezaji wako. Hata hivyo kama ilivyo kawaida ya bima zote mfumo huu unakurudishia gharama zako tu ulizotumia bila faida. Na muda wa kulima utapofika wakati unaomba mkopo utajaza hiyo fomu ya bima pia

Nimekopa mkopo JATU Saccoss wa Millioni 10 lakini baada ya mavuno nimepata Millioni 8, JATU itanisaidiaje kurecover mkopo?

Ndio mkuu kuna bima na mkulima anapochukua tu mkopo wake wa kilimo atasaini Insuarance policy hivyo kukusaidia kipindi cha changamoto kama hiyo

Kwa hapa kiteto mashamba yenu na ofisi zipo wapi

Nenda hapo stend kuu (kibaya) utaona bango la Jatu. Pia mashamba yetu yapo pori namba moja hapo pamoja na Matui

Ehh Sasa mmechagua kutumia kilimo cha umwagiliaji au ya mvua?

Kilimo cha Umwagiliaji ndo mpango wa JATU kwa mashamba yote lakini inahitaji subira kufika huko ndo tumeanza mwaka huu tunaamini ifikapo 2022 tutakuwa na mashamba makubwa ya Umwagiliaji. Kwa sasa ni muhimu tulime kwa kutegemea mvua maana pia tunapata uzoefu na malighafi kwa ajili ya viwanda chetu

Nimeona kuna aina tofauti za UANACHAMA na kila moja Ina vigezo na masharti. Je hii uliyotupa hapa ufafanuzi ni aina gani ya uanachama? Na Je swali langu kuna gawio?  Kule kwenye kampuni?

Hapa ni wanachama wanahisa (mwanachama mwanahisa) ambaye unaruhusiwa kushiriki kwenye kilimo pia. Kuhusu gawio unapata gawio kila mwaka kutokana na hisa zako kwa kuzingatia faida ambayo kampuni imetengeneza lakini pia unapata gawio la faida kila mwezi kutokana na manunuzi ya bidhaa unayofanya kupitia app ya JATU

Je naweza jiunga JATU kwaajili tu ya kununua bidhaa na sitaki kushiriki kwenye kilimo?

Ndio, unaweza nunua bidhaa za JATU kupitia kwa mawakala wetu au kupitia app ya JATU na utapata gawio kwa kila bidhaa utayonunua

Huku naona kuna some sort of NETWORK MARKETING, hii imekaaje?

Mfumo wa masoko wa JATU ni wa network marketing kila mteja atayejiunga na JATU inabidi anufaike na gawio la faida la bidhaa zetu hivyo kila mteja atakua na watu chini yake atakaowaunga JATU nao watapata gawio kutokana na manunuzi yao

Mpaka sasa mshalima miaka mingapi na matokeo yapoje?

Tumelima toka mwaka 2017 na matokeo kwa misimu miwili sasa ni mazuri katika zao la mahindi, maharage, mpunga na alizeti na mwezi huu ni mwezi wakuanza mavuno tutawajulisha mavuno yatakuaje, naamini kila mmoja atavutiwa kulima na JATU. Maana ni gharama kidogo, nguvu kidogo lakini faida ni kubwa.

Hisa zina faida gani?

Kama zilivyokampuni nyingine za umma, hisa katika JATU nimtaji. Na wewe kama ukinunua hisa ndani ya JATU manaake umeamua kuwekeza JATU na unakuwa mmoja wawamiliki wa kampuni. Lakini faida zingine ni kushiriki kwenye kilimo na miradi mingine ya JATU nje ya faida ya gawio kila mwaka

Je kwa sasa mazao mnayodeal nayo ni Mahindi, Alzeti, Mpunga na Maharage tu?? Na mahitaji ya utunzaji yanatofautiana vipi?? Mnafikiri kwenda kwenye mazao mengine kama Vitunguu, Viazi n.k

Kila zao lina utaratibu wake wa utunzaji JATU hutoa mchanganuo wa kila zao linapolimwa hivyo tutawajulisha kuhusu hayo mengine msimu wake utapofika. Lengo la JATU ni kuwekeza kwenye kilimo na viwanda hivyo hatuna mipaka ila kwasa kwakua safari ni hatua tumeanza na hayo mazao lakini kadri tunavyozidi kukua ndo tunavyozidi kuongeza mazao baada ya utafiti wa kina

Je inawezekana nisiwe mwanachama, yaani nisideal na nyie, nikalima mwenyewe na huduma zingine zote nikafanya mwenyewe hadi mavuno, then JATU ikanisaidia kupata soko??!

Hapana, ili uweze kunufaika na fursa zetu ni lazima uwe mwanachama wa JATU

Mwisho wa kuweka oda kwa kilimo cha mahindi ni lini?

Mwisho wa kuweka oda kwa kilimo cha mahindi ni tarehe 30 Juni 2019