MASHAMBA YA JATU

JATU PLC kwa kushirikiana na wanachama wake inamiliki mashamba makubwa matatu mpaka sasa ambayo yanapatikana mikoa ya Manyara, Tanga na Morogoro.

Wilayani Kiteto, Manyara JATU inafanya kilimo cha mahindi ambapo zaidi ya ekari 1000 tayari zimelimwa ambapo mpaka 2022 kutakua na jumla ya ekari 2500 za kilimo.

Pia Wilayani Kiteto, Manyara JATU inafanya kilimo cha alizeti ambapo zaidi ya ekari 1000 tayari zimelimwa ambapo mpaka 2022 kutakua na jumla ya ekari 2500 za kilimo.

Wilayani Kilindi, Tanga JATU inafanya kilimo cha maharage ambapo zaidi ya ekari 200 tayari zimelimwa ambapo mpaka 2022 kutakua na jumla ya ekari 1000 za kilimo.

Kwa upande wa wilaya ya Kilombero, Morogoro JATU imejikita kwenye kilimo cha mpunga ambapo mpaka sasa ekari zaidi ya 200 zishalimwa na kampuni inaendelea kuwekeza ambapo mpaka 2022 kutakua na ekari takribani 1000 zimelimwa.