Kilimo cha Mpunga

JATU PLC inawakaribisha wanachama na wadau wa kilimo kuweza kushiriki kwenye mradi wa kilimo cha mpunga kwa msimu huu wa mwaka 2019/2020 ambapo maandalizi yameanza kufanyika. Msimu huu JATU kwa kushirikiana na wanachama wake imejipanga kufanya kilimo cha mpunga kwenye mikoa ya Morogoro kwa takribani ekari 1000 na Shinyanga ambapo tutalima ekari 500. Kumbuka ukilima na JATU inakuhakikishia usimamizi uliobora na utumiaji wa nyenzo za kisasa za kilimo ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima wetu. Pia JATU inatoa mikopo kwa wakulima ambao wamejiunga kwenye mfuko wetu wa akiba wa JATU Saccos na kuweka angalau 1/3 ya gharama zote za kilimo nawe utakopeshwa kiasi kilichobaki.

Zao: MPUNGA
Mmiliki: MWANACHAMA WA JATU
Msimamizi: JATU PLC
Eneo: MBINGU, MOROGORO na KAHAMA, SHINYANGA
Muda: JULY 2019 -MAY 2020

mchanganuo wa gharama za kilimo kwa ekari 1

 1. Kukodi shamba~100,000/-
 2. Kulima round 1 (kukatua) ~45,000/-
 3. Kulima round 2 ~45,000/-
 4. Kupiga hallow ~30,000/-
 5. Kupanda (planter)~50,000/-
 6. Dawa (2-4D) 1lt. ~20,000/-
 7. Ng’olezi ~60,000/-
 8. Mbolea (CAN +Urea) ~100,000/-
 9. Kuvuna (combined) ~150,000/-
 10. Usafiri na mifuko ~100,000/-
 11. Usimamizi (JATU) ~100,000/-
 12. Tahadhari ~40,000/-

JUMLA KUU = TSHS. 840,000/-

MATARAJIO YA MAVUNO
—————————————
Kwa ekari moja iliyosimamiwa na kuhudumiwa kitaalamu inaweza kutoa kati ya gunia 18-30 za Mpunga; ambapo gunia la debe 8 linaweza kutoa kati ya kg 65-75.

BEI YA MCHELE
Mkulima anashauriwa kukoboa mpunga wake kupitia viwanda vya Jatu ili aweze kupata mchele mzuri ambao ataweza kuuza kwa bei nzuri sokoni. Bei ya mchele wakati wa mavuno ni kama ifuatavyo:

MCHELE GRADE ‘A’~1,300-1,400/-@Kg
MCHELE GRADE ‘B’~1000-1200/-@kg

Mkulima akivumilia ili auze mchele wake kuanzia mwezi wa Tisa grade B inaweza ikawa imefika bei ya tshs. 1500/- kwa kila kg moja.

Hivyo basi; tukadirie bei ya kawaida ya mchele itakuwa 1500/- kwa kg 1 na kwamba mkulima anaweza kuvuna gunia 18 za mpunga zenye debe 8 Sawa kg 70 za mchele. Hii ni sawa na:

Gunia 20 x kg 70 x Tshs. 1500/- =2,100,000/- kama mapato ya ekari 1

FAIDA TARAJIWA KWA EKAR 1
————————————————
Ili kupata faida ya ekari 1 ya mpunga kwa makadirio ya hapo juu; ni sawa na;

2,100,000 – 840,000/- = 1,260,000/-

Bonyeza link hapa kujiunga na group la taarifa juu ya kilimo hichi cha mpunga

Open this link to join my WhatsApp Group: https://chat.whatsapp.com/GqbZuhrrHH01ztAYwsfMHw

Angalizo:
Faida hiyo ni makadirio ya kawaida kwa kilimo hichi; Hata hivyo yanaweza kupanda au kushuka kwa kutegemeana na Hali halisi ya hewa na mazingira kwa ujumla.

Jatu~jenga afya tokomeza umaskini