Kilimo cha Mahindi

JATU inawatangazia wanachama wake kuwa msimu mpya wa kilimo cha mahindi umeanza na maandalizi yameanza kufanyika, hivyo kuwataka wale wote ambao wangependa kushiriki kutoa taarifa kwa kupiga simu kwenda namba 0768 342 943. Kilimo cha mahindi kitafanyika kwenye mashamba yetu jumuishi yanayopatikana wilayani Kiteto, Manyara. Zaidi ya ekari 500 zinategemewa kulimwa kwa kushirikiana na wanachama ambao ni wadau wa kilimo. Kumbuka ukilima na JATU inakuhakikishia usimamizi bora na utumiaji wa vifaa vya kisasa vya kilimo hivyo kukupatia mavuno yalio na tija na ya uhakika.

MCHANGANUO WA KILIMO CHA MAHINDI KITETO, MANYARA

———————————————

Zao: MAHINDI YA KAWAIDA
Mmiliki: MWANACHAMA WA JATU
Msimamizi: JATU PLC
Eneo: KITETO,MANYARA
Muda: JULY 2019 -MAY 2020

UTANGULIZI
———————
JATU PLC ni kampuni ya Umma ambayo imejikita katika kumsaidia mkulima kupata shamba, kulima kisasa na kuvuna mazao kwa gharama nafuu, pia kampuni ina msaidia mkulima kupata soko la uhakika kwa mazao yake yote ambayo analima kwa usimamizi wa JATU. Bei ya mazao jatu ni bei elekezi ya serikali ambayo haina madalali ndani, mkulima hana haja ya kuhangaika na usimamizi wa shamba Kwani kampuni ina wataalamu na vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kilimo bora.

Zao la mahindi ni muhimu JATU kwa sababu linaisaidia kampuni kupata malighafi kwa ajili ya kiwanda chake ambacho kinazalisha unga wa mahindi Dona na sembe. Mwakani tunategemea ukuaji mkubwa sana kwa kampuni yetu na hivyo tunalazimika kulima mahindi kwa sehemu kubwa ili kujihakikishia malighafi za kutosha kiwandani kwetu. Hii pia ina mhakikishia mkulima wetu soko.

GHARAMA ZA KULIMA MAHINDI
————————————————
Hizi gharama zimegawanyika katika sehemu kuu sita (6) kama ifuatavyo;

 1. KUKODI SHAMBA
  -Gharama ya ekari 1~35,000/-
  -Gharama ya usafiri ~10,000/-
  -Gharama ya JATUApp ~5,000/-
  JUMLA NDOGO~50,000/-
 2. KULIMA SHAMBA EKARI 1
  -Kulima awamu ya 1 ~30,000/-
  -Kulima awamu ya 2 ~30,000/-
  Jumla ndogo~ 60,000/-
 3. KUPANDA MAHINDI
  -Kupiga hallow na kupanda kwa planter ~ 30,000/-
  -Mbegu kg 10~ 60,000/-
  -Mbolea kg 50 (DAP)~ 58,000/-
  JUMLA NDOGO ~ 148,000/-
 4. PALIZI
  -Awamu ya 1 ~ 30,000/-
  -Awamu ya 2 ~30,000/-
  -Mbolea ya kukuzia (urea) kg 50~ 48,000/-
  JUMLA NDOGO~ 108,000/-
 5. DAWA
  Dawa ya kuua vimelea na wadudu ~35,000/-
 6. KUVUNA GUNIA 1 ya MAHINDI
  -Kuchuma mahindi ~1000/-
  -kupukuchua~2,000/-
  -Mfuko wa kuhifadhia – 35000/-(pics)
  -kujaza mfuko ~500/-
  -kupima na kushona mfuko~500/-
  -Usafiri kutoka shamba hadi store~5000/-
  -Kupakia na kushusha gunia~1000/-
  -Ushuru wa serikali ~1500/-
  JUMLA NDOGO~14,000/-

MAKADILIO YA MAVUNO KWA EKARI 1
—————————————————
Inakadiriwa ekari moja ikihudumiwa vizuri kwa kuzingatia hatua zote kama nilivyotaja hapo juu, na hali ya hewa ikawa nzuri; mkulima anaweza kupata kati ya Gunia 30-35 za ujazo wa kg 90.

Kama ndivyo; maana yake gharama za kuvuna zitategemeana na kiasi cha magunia; kwa mfano hapo kama tukiweka gunia 30 gharama ya kuvuna itakuwa Sawa na 30 x 14,000/-

Ambayo ni; 420,000/- 
Hii ndo gharama ya kuvuna ekari moja, sasa ili kupata gharama ya mradi mzima kwa ekar moja kuanzia kukodi hadi kuvuna tunajumlisha kama ifuatavyo;

 1. kukodi ~50,000/-
 2. Kulima~60,000/-
 3. Kupanda~148,000/-
 4. Palizi~108,000/-
 5. Dawa~35,000/-
 6. Kuvuna ~420,000/-
 7. Usimamazi (JATU) ~50,000/-
 8. Tahadhari: ~ 29,000/-
  ————————————————
  JUMLA KUU: 900,000/- Tshs.

MATARAJIO YA FAIDA
———————————
Tukitumia bei ya kawaida kabisa ambayo ni ya uhakika Tshs. 500/- kwa kg moja ya Mahindi, na tukachukulia kiwango cha chini kabisa cha gunia 30 za kg 90 kwa ekari moja, tunategemea kuuza mazao yetu jumla ya tshs. 
30x90x500=1,350,000/-

Ili kupata faida: 1,350,000 – 871,000/-
=479,000/-Tshs.

Hii ndo kadirio la faida kwa ekar 1 
————————————————

Mkopo wa JATU Saccos hauna riba na mkulima anakopeswa 2/3 ya gharama zote. Kwa mujibu wa gharama zetu kwa ekari moja hapo juu inaonesha 1/3 ambayo mkulima anatakiwa kuchangia ni 291,000/=

Maelezo hayo ni makadario ya mradi wa kilimo cha mahindi kinachoweza kusimamiwa na JATU PLC katika eneo la kiteto mkoa wa Manyara, tumepata gharama hizo kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kilimo hicho Kwani tumeshawahi kulima zao hilo katika wilaya hiyo na hivyo tunajua mahitaji yote pamoja na changamoto na njia za kukabiliana nazo ili kuhakikisha mkulima anapata faida tarajiwa. Kwa uzoefu na Imani ya timu ya jatu tunaamini tutamwezesha mkulima kufikia lengo hilo, hata hivyo tunawataka wakulima wote wajue kwamba kilimo kina changamoto na fursa nyingi na kuna uwezekano wa makadilio hayo ya faida kuongezeka au kupungua kutegemeana na Hali halisi ya kilimo kwa wakati husika.

Kama bado hujajiunga katika mradi wa mahindi JATU-KITETO jiunge katika group letu la whatsapp upate maelezo kamili ya mradi huu ili uweze kushiriki na kutengeneza faida. Njoo ujue namna ya kulima kisasa na namna ya kupata mashamba kwa bei nafuu kwa kukodi au kununua na JATU inasimamia huduma zote kuanzia shambani hadi wakati wa kuvuna utavuna na kulipa mkopo wako ambao utakopeshwa kwaajili ya kulima na JATU bila riba. Usisahau kusambaza link hii kwa watanzania wenzetu

https://chat.whatsapp.com/JzVJ9txNaXe4M7qdTUCdQG

Imetolewa tarehe 07.06.2019
JATU PUBLIC LIMITED COMPANY 
————————————————

Jenga Afya Tokomeza Umaskini~JATU