JATU DIASPORA

SABABU ZA DIASPORA KUJIUNGA NA HUDUMA ZA KAMPUNI YA JATU PLC
—————————————————

Tunaendelea kutoa shukrani zetu za dhati kwa wanadiaspora wote ambao walikua nasi bega kwa bega katika mchakato mzima wa IPO, taarifa njema ni kwamba tumeweza kufanikisha lengo kwa asilimia 104.

Hivyo basi tunaendelea kuwaasa kushiriki katika miradi mbalimbali inayopatikana katika kampuni ya JATU PLC ambapo tunaendelea na kampeni ya ANZA NA EKARI MOJA ikiwa na lengo la kuwahamasisha wanachama wetu kushiriki katika miradi tofautitofauti, kama kilimo cha mpunga ambacho kinafanyika mkoani Morogoro, kilimo cha mahindi na alizeti mkoani Kiteto Manyara, kilimo cha maharage kilichopo mkoani Tanga, lakini pia kilimo cha ngano kilichopo wilaya ya Sumbawanga, kilimo cha machungwa wilaya ya handeni mkoani Tanga na kilimo cha parachichi kilichopo mkoani Njombe.

Kwa mwanachama ambaye atakua anataka kushiriki kilimo chini ya usimamizi wa JATU PLC kuanzia ekari 1 mpaka 49 watalima kwa uwiano wa 1:50 yaani hisa 50 kwa ekari 1 na kwa wale wakulima wote ambao wataanzia ekari 50 na kuendelea watalima kwa uwiano wa 1:500 yaani hisa 500 kwa ekari 1.

Jatu inachukua nafasi hii kuwajulisha kwamba kampuni baada ya kufanikisha kuuza hisa zake kupitia ofa iliyotolewa kuanzia tarehe 01.06.2021 hadi tarehe 15.07.2021 sasa kuna uhakika wa kuboresha miundombinu ya kilimo kwa kununua vifaa vingi na vya kisasa kama vile trekta, mashine za kuvunia na kulima pamoja na kujenga miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji na viwanda.

Tunawajulisha kwamba kwa msimu unaofuata tutaanzisha miradi mipya ya kilimo ambao ni kilimo cha mbogamboga katika eneo la kimbiji wilaya ya Kigamboni, kilimo cha maembe katika wilaya ya Chalinze kijiji cha Masimbani na mazao mengine mengi kadri tutakavyo pokea mawazo ya wanachama kupitia JATU TALK.

JATU,Jenga Afya Tokomeza Umaskini.