HABARI

FURSA YENYE KUWAFIKIA WOTE

Kampuni ya JATU inazidi kutangaza fursa ya HISA kwa watanzania ikiwa na dhima ya kuwafikia watu wote wenye kipato cha chini, kipato cha kati na kipato cha juu. Kupitia kampeni ya BUKU TANO INATOSHA, tumekua tukiwafikia wananchi wengi zaidi ambapo kwa siku ya leo kampeni hii imefanyika maeneo ya Sinza, Bunju, Mbezi ya Kimara, Kinondoni na Magomeni pamoja na viunga vyake, kesho tutakua wapi…?

Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii. Kununua hisa za JATU ili uweze kunufaika zaidi, hisa moja inauzwa shilingi 500, BUKU TANO INATOSHA kumiliki hisa 10 ndani ya kampuni ya JATU.

JATU PLC YATAMBULISHA RASMI MABALOZI WA BUKU TANOINATOSHA

Kampeni ya BUKU TANO INATOSHA ilizinduliwa rasmi tarehe 5 Julai 2021 katika viwanja vya maonyesho sabasaba ambapo lengo la kampeni hii ni kuifahamisha jamii nzima kuwa kampuni ya JATU ipo katika uuzaji wa hisa zake za awali ambapo kwa BUKU TANO(elfu tano) tu unakua umenunua hisa 10 za JATU na kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni.

Leo siku ya Tarehe 11/6/2021 Uongozi mzima wa JATU PLC uliwatambulisha rasmi mabalozi wa kampeni ya BUKU TANO INATOSHA mbele ya waandishi wa habari, na kila balozi alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari, mabalozi hawa walitoa shukrani zao za dhati kwa uongozi wa JATU  kwa kuwaamini lakini pia walipata nafasi ya kueleza namna ambavyo watakua mabalozi wazuri wa kampeni hii ya BUKU TANO INATOSHA kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi atapata kufahamu fursa hii bila kujali kipato chake kwani BUKU TANO INATOSHA kuwekeza ndani ya JATU kwa kununua hisa.

Mabalozi waliotamblishwa siku ya leo ni pamoja na Dokii Wenceslaus, Maufundi, Mwijaku, Tabu Mtingita, Piere Likwidi na Anthony Luvanda maarufu kama Mc Luvanda.

Tarajia kukutana na mabalozi hawa mtaani kwako kuanzia sasa kwani JATU PLC kupitia kampeni ya BUKU TANO INATOSHA imekua ikipita mtaa kwa mtaa ambapo maafisa masoko  wa kampuni  wamekua wakitoa elimu zaidi juu ya hisa, lakini pia unaweza kununua hisa za JATU kupitia matawi yote ya benki ya NMB, DCB, Matawi yote ya ofisi za JATU, mawakala(brokers) na Dar es salaam Stock of Exchange(DSE).

UZINDUZI WA KAMPENI YA BUKU TANO INATOSHA

Rasmi kampuni ya Jatu Plc leo imezindua kampeni yake ya Buku Tano Inatosha ndani ya viwanja vya Mwl. Nyerere sabasaba maonyesho, ambapo shughuli ilianza saa tatu kamili asubuhi ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Jatu Plc Ndg. Peter Isare Gasaya ambapo kampeni hii inahusiana na uzinduzi wa uuzaji wa awali wa hisa za Jatu ndani ya soko la hisa ambapo hisa moja ni shilingi mia tano, hivyo kwa shilingi elfu tano utakua una uwezo wa kumiliki hisa kumi za Jatu Plc.

Faida za kumiliki hisa za Jatu ni pamoja na kushiriki katika miradi ya kilimo ndani ya Jatu, kupata gawio la faida kila mwaka kutoka kwenye faida itakayoipata kampuni, kupata uwakala wa huduma za Jatu kama vile kuuza bidhaa za Jatu na utapata gawio la faida kutoka kwenye kila bidhaa utakayouza na kuwa mwanachama mnufaika wa Jatu saccos Ltd, pia unaweza kupata mikopo ya kilimo bila riba na mikopo mingine ya maendeleo.

Uuzaji wa awali wa hisa za Jatu utafanyika kwa siku arobaini na tano ambapo fomu hizi zinapatikana katika matawi yote ya benki ya NMB, benki ya DCB, madalali (brokers), Maafisa masoko wa Jatu Plc ambao watakua wanapatikana mitaani pamoja na matawi yote ya ofisi za Jatu Plc, yaani; Dar es salaam, Mwanza, Mtwara, Arusha pamoja na Dodoma.

MKUTANO WA MKURUGENZI NA WAKULIMA WA JATU PLC

Ni mkutano maalum ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Jatu Plc, Ndg. Peter Isare unaolenga kukutana na wakulima wa Jatu Plc kujadili mambo mbalimbali yanayohusu huduma zetu ikiwemo; Kufahamu mfumo wa malipo ya mazao ya wakulima, Taarifa kuhusu mavuno ya msimu wa mwaka 2020/2021, Mwenendo wa maandalizi ya msimu ujao wa mwaka 2021/2022 pamoja na mengineyo.

Mkutano huu utafanyika siku ya Jumamosi hii ya Tar 5/6/2021 katika viwanja vya Mwl. Nyerere, Sabasaba Maonyesho, Kuanzia saa Tatu Kamili Asubuhi. Usipange kukosa, na hakuna kiingilio.

NYOTE MNAKARIBISHWA….!

JATU PLC NA KILIMO CHA ALIZETI

Alizeti ni zao linalolimwa kwa wingi nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Duniani kote kwa Ujumla. Alizeti hulimwa kwa wingi karibu maeneo yote nchini Tanzania katika nyanda za kaskazini, kati, mashariki pamoja na nyanda za juu kusini hasa katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara na Rukwa. Hii inatokana na uwezo wa alizeti kustawi vizuri katika mazingira mengi tofauti bila ya kuwa na utofauti mkubwa katika uzalishaji wake.

Alizeti ni zao la kibiashara na ni moja kati ya mazao matano yanayolimwa ndani ya kampuni ya JATU PLC kwa takribani miaka mitano mfululizo toka kuanzishwa kwa shughuli za kilimo katika kampuni ya JATU PLC ambalo hutumika kuzalisha bidhaa ya mafuta ya kupikia yaani JATU COOKING OIL.

Mbegu za Alizeti zinapokamuliwa hutoa mafuta yanayoweza kutumika kwa matumizi mbalimbali hasa kupikia. Wataalamu wengi wa afya wanapendekeza matumizi ya mafuta ya alizeti katika mapishi kwa sababu hayana lehemu na hivyo ni salama kiafya hasa yanapotumika vizuri. Kwa sababu hiyo mafuta yanayotokana na alizeti yamekuwa na soko zuri na hivyo biashara yake ni njia nzuri ya kumwongezea mkulima na mfanyabiashara kipato.

Katika msimu wa mwaka 2020-2021 JATU PLC ilianza maandalizi ya mashamba ya alizeti mwishoni mwa mwezi Septemba na kuanza shughuli rasmi za kupanda kufikia mwezi Novemba ambapo takribani zaidi ya ekari 1000 zililimwa na kupanda mbegu chotara aina ya AGUARA 4 ambayo ni mbegu fupi inayotengeneza vichwa vyenye kuzaa mbegu nyingi na mavuno yake huwa ni mazuri, pia inakomaa mapema kwa wastani wa siku 86 hadi 95, ina kiwango kikubwa cha mafuta cha 40% na pia ina uwezo wa kujikinga na ndege kutokana na tabia ya kichwa kutazama kuelekea chini.

Kwa sasa Wataalamu kutoka shambani wanaendelea na utekelezaji wa kusimamia zao hili kwa umakini mkubwa kwa lengo la kumpatia mkulima wa JATU mavuno ya kutosha na baadae apate faida nzuri baada ya kuuza mazao yake kwenye viwanda vya JATU.

Karibu kuwekeza katika msimu ujao kwani mashamba yanapatikana kupitia JATU MARKET APP inayopatikana Playstore na Appstore. Wahi mapema ununue na ukodi mashamba kadhalika kujihakikishia kupata mkopo wa kilimo usiokuwa na riba kutoka JATU SACCOS.

JATU

Jenga Afya, Tokomeza Umaskini

MUENDELEZO WA SEMINA ZA JATU

Jatu Plc inayofuraha kukuletea Semina Maaalum itakayofanyika Tar. 22 May 2021, semina hii itafanyika katika ofisi za Jatu Makao Makuu, Posta Barabara ya Samora, Jengo la PSSSF House ghorofa ya 11, muda ni kuanzia Saa Nne Asubuhi.

Njoo ujifunze na kufahamu fursa mbalimbali zipatikanazo ndani ya Jatu Plc. Usisubiri kuhadithiwa, karibu ujiunge na ulimwengu wa fursa mbalimbali za uwekezaji katika Kilimo, Viwanda na Masoko.

SEMINA HII NI ZAIDI YA JANA.

Na Hakuna kiingilio…..! Nyote Mnakaribishwa.