Ndugu mwanachama wa JATU ambae ungependa kushiriki fursa yetu ya uwakala hakikisha umesoma vigezo na masharti vya uwakala kabla ya kujaza fomu hii:
Vigezo na masharti ya uwakala wa JATU:
- Lazima awe mwanachama wa JATU
- Lazima awe na smartphone au computer
- Awe tayari kununua kuanzia hisa 50 na kuendelea za JATU PLC soko la hisa likifunguliwa
- Awe na sehemu ya biashara iliotengwa kwaajili ya kutoa elimu ya JATU na mauzo ya bidhaa
- Awe na leseni ya biashara/TIN
- Awe mwanachama wa SACCOS na awe na akiba kuanzia laki 3 na kuendelea.
- Awe na chombo chake cha usafiri au ukaribu na mtu mwaminifu mwenye chombo cha usafiri
- Awe na cheti cha mafunzo ya ubalozi cha JATU