MATANGAZO MUHIMU

MKUTANO WA CEO NA WAKULIMA WA JATU PLC

 Ndugu wakulima na wanachama wote wa Jatu Plc.Tunapenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na mkutano maalumu wa mkurugenzi akiongea na wakulima wa Jatu Plc.

TANGAZO LA KAZI YA AFISA MAUZO

Kampuni ya JATU PLC inatoa fursa kwa vijana wa Kitanzania walio katika mikoa ifuatayo: Dar Es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mtwara na Arusha kwa nafasi za Afisa Masoko.

Taarifa Maalumu kwa wanachama wa Jatu Plc kuhusiana na Mabadiliko ya Muda wa Kazi.

Tangazo kwa wanachama wakulima walioweka ahadi ya kulipia mashamba baada ya kuuza mazao.

Tangazo muhimu kwa wanachama wa JATU wanaomiliki mashamba ya kununua Kiteto, Manyara.

Habari, Tunapenda kuwatangazia wanachama wote wa Jatu na ambao sio wanachama wanategemea kuwa miongoni mwa familia ya Jatu, kumekuwa na uvumi wa taarifa ambazo sio sahihi, zikihusisha uwekezaji na ulipaji fedha wa madawa ya kilimo na uchimbaji wa madini. Taarifa hizi hazina ukweli wowote ule na Jatu haiwatambui hawa watu na hawana mikataba yoyote au ushirikiano wa kibiashara baina yao na kampuni.

Kampuni inatoa onyo kali kwa wanachama na kuwatahadharisha kwamba usitume fedha kwa namba ya simu ya mtu yeyote yule kama sio namba ya kampuni au Akaunti namba za Benki za Jatu Plc kwa ajili ya usalama wa fedha zako. Matukio haya huendeshwa na baadhi ya wanachama ambao wanatoa taarifa kwa watu na kutumia namba ambazo hazipo jatu.

Idara ya masoko ya JATU PLC inapenda kuwatangazia umma na wanachama kuwa tumefungua ofisi mpya ya idara ya masoko ambayo kila Jumamosi itakua ikiendesha semina za elimu kuhusu huduma na fursa kupitia kampuni yetu. Pia tunakaribisha maombi ya kazi za afisa masoko wa JATU kwa vijana wenye elimu ya kuanzia Diploma na kuendelea walete CV zao ofisi zetu zilizopo Posta mtaa wa samora jengo la PPF House ghorofa ya 6 na ukumbi wa semina upo ghorofa ya 11. Nyote mnakaribishwa

Baada ya zoezi ya uuzaji hisa za ndani za JATU PLC kusitishwa hadi hapo soko litapofunguliwa kupitia DSE zoezi zima la ununuaji wa mashamba na kujiunga na JATU Saccos na kuweka akiba linaendelea kama ilivyokua awali, lakini baada ya DSE kila mwanachama mwenye shamba au kajiunga na JATU Saccos atalazimika kununua hisa ili kukamilisha vigezo