KARIBUNI KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAVUNO

JATU PLC ikishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo tunaendelea na maonyesho ya Kilimo ya Kikanda katika Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi ambapo leo hii tarehe 13.09.2021 ndio uzinduzi rasmi wa maonyesho haya yatakayofanyika katika viwanja vya Uhuru Pack huku Mgeni rasmi akiwa ni mheshimiwa Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini.

Kumbuka maonyesho haya ni bure hakuna kiingilio, karibu ufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya JATU, vilevile utapata elimu zaidi kuhusu maana halisi ya Anza na ekari Moja na namna ambavyo unaweza kufanya kilimo kisichokua na stress chini ya usimamizi wa JATU, pia kutakua na maafisa ugani zaidi ya 100 watakaotoa elimu zaidi kuhusu kilimo bora pamoja na masuala ya mbegu, lakini pia utapata kujionea mashine mbalimbali za kilimo.

Maonyesho haya yatasindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Mrisho Mpoto pamoja na band yake, bila kuwasahau wasanii maarufu wa bongofleva kama ndege mnana “Linah Sanga” na Barnaba Classic pamoja na wengine wengi.

Usisahau kutembelea YouTube channel yetu JATUTALK TV ili kupata habari zaidi.

WIKI YA MAVUNO NDANI YA KILIMANJARO

Jatu Plc kupitia kampeni ya WIKI YA MAVUNO, ANZA NA EKARI MOJA bado tunaendelea kuhakikisha wakazi wa Kanda ya Kaskazini wanaendelea kunufaika na fursa zilizopo ndani ya Jatu plc, siku ya jana ilikua ndio kilele cha kampeni hii ndani ya mkoa wa Arusha ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa na kuacha alama chanya kwa wakazi wa Arusha, wengi walijiunga na Jatu kwa kuanza na Ekari moja pia kuahidi kuwa watakuwa mabalozi wazuri wa kampuni ya Jatu.

Jatu Plc bado tunaendelea na kampeni hii Kanda ya Kaskazini. Kilimanjaro ndio mkoa unaofuata ambapo maonyesho haya yataanza rasmi tarehe 13.09.2021 mpaka 19.09.2021 timu nzima ya Mpoto Band ikiongozwa na Mrisho Mpoto maarufu kama “Mjomba” watakuwepo kutoa burudani na kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa wanakilimanjaro kwa njia ya sanaa lakini pia meneja mkuu wa Jatu Plc Bw. Mohammed Issa Simbano atakuwepo kuhakikisha kutoa darasa lenye kuwaelimisha wakazi wa kaskazini kuhusu kilimo chenye tija kinachofanyika ndani ya Jatu Plc kwa kuanza na ekari moja.

Usisahau kutembelea YouTube channel ya JATU TALK TV pamoja na Instagram jatu_plc ili kupata taarifa zaidi.

HISA ZA JATU PLC ZAREJEA SOKONI

Kampuni ya Jatu Plc kupitia soko la hisa la Dar es salaam (DSE) tunapenda kuwajulisha kuwa leo Tarehe 31.08.2021 hisa za Jatu Plc zimerudi sokoni rasmi kwa kishindo kikubwa huku zikitarajiwa kulichangamsha soko la hisa kutokana na uhitaji wa hisa hizo sokoni, huu ndio wakati sahihi kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kununua hisa za Jatu katika kipindi cha ofa ya buku tano inatosha.

Hivyo basi, tunawakaribisha kununua hisa za jatu ambazo zinakufanya kukidhi vigezo vya uwekezaji ndani ya Jatu Plc, kama vile kushiriki katika miradi ya kilimo, lakini pia kufunguliwa kwa soko la hisa kunatoa nafasi kwa wale ambao walinunua hisa kuziuza kwa bei ya juu ili wapate faida zaidi mara baada ya hisa kupanda bei.

Hisa za Jatu plc unaweza kuzinunua kupitia madalali rasmi wa soko la hisa wanaopatikana Dar es salaam au unaweza kununua kupitia mfumo wa DSE kiganjani.

Kumbuka kigezo kikubwa cha kufanya kilimo ndani ya Jatu Plc ni lazima kumiliki hisa 50 kama utahitaji kulima ekari 1 mpaka 49 ambayo ni sawa na uwiano wa 1:50 na mkulima anayetaka kulima ekari 50 na kuendelea anatakiwa kuwa na hisa 500 kwa kila ekari yaani 1:500, kampeni ya ANZA NA EKARI MOJA bado inaendelea na huu ndio muda sahihi wa kuendelea kununua ama kukodi mashamba ndani ya Jatu Plc.

Kwa maswali au maelezo zaidi kuhusu hisa wasiliana nasi kupitia namba: 0758 495271

LIMA BILA STRESS NA JATU PLC

MAONYESHO YA WIKI YA MAVUNO YAANZA RASMI MKOANI ARUSHA

JATU PLC tunapenda kuwakaribisha wananchi wote wa Arusha Pamoja na maeneo ya jirani katika ufunguzi wa maonyesho ya WIKI YA MAVUNO, ANZA NA EKARI MOJA yanayoanza rasmi  leo Tarehe 30.08.2021 mpaka Tarehe 05.09.2021 katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha. Lengo kuu la maonyesho haya ni kutoa elimu zaidi kuhusu Kilimo huku JATU PLC tukiwa na kauli mbiu ya ANZA NA EKARI MOJA.

Katika maonyesho haya viongozi mbalimbali watahudhuria, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Bi. Sophia Mjema, Pamoja na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kama Tanzania Agriculture Research Institute (TARI), EAST WEST, AGRICOM na EFTA lakini pia maonyesho haya yatasindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Mrisho Mpoto (Mjomba) na  bendi yake pamoja na msanii Joh Makini (mwamba wa kaskazini).

Timu nzima ya Jatu Plc ikiongozwa na Meneja Mkuu Bw. Mohammed Issa Simbano itakuwepo kuhakikisha kuwa kila mwananchi ananufaika na maonyesho haya kwa kupata elimu zaidi kuhusiana na fursa zinazopatikana ndani ya Jatu Plc.

Kampeni hii ya WIKI YA MAVUNO, ANZA NA EKARI MOJA inatarajiwa kugusa mikoa mbalimbali kanda ya kaskazini kama vile Tanga, Kilimanjaro pamoja na Manyara.

Tembelea youtube channel yetu; JATUTALK TV kwa taarifa na matukio mbalimbali yanayoendelea ndani ya Jatu Plc.

KUELEKEA WIKI YA MAVUNO KANDA YA KASKAZINI

Kampuni ya JATU PLC ikiongozwa na Meneja Mkuu Bw Mohammed Issa Simbano imewafikia wakazi wa Arusha tukiwa na kampeni iliyopewa jina la WIKI YA MAVUNO, ANZA NA EKARI MOJA kampeni hii ina lengo la kuwahabarisha zaidi wakazi wa Arusha na kanda nzima ya kaskazini yaani Kilimanjaro, Tanga na Manyara kuhusu shughuli zinazofanywa na JATU PLC hususani katika suala zima la Kilimo.

Washiriki mbalimbali wata kuwepo, ni pamoja na wadau wa sekta ya kilimo.

Wote mnakaribishwa kuwekeza ndani ya Jatu Plc. Karibu tulime bila Stress.

MKUTANO MKUU WA WAKULIMA WA JATU PLC JIJINI DAR ES SALAAM

Kuelekea katika siku ya wakulima ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 mwezi wa 8 kila mwaka, kampuni ya JATU leo tarehe 7/8/2021 imefanya mkutano katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel Ubungo Plaza na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 1500 huku ajenda kuu zikiwa ni mrejesho wa kilimo 2020/2021, mwenendo wa hisa za JATU na ufunguzi wa miradi mipya ya Jatu Plc.

Mkutano huu uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa JATU PLC Ndg. Peter Isare Gasaya, lakini pia Meneja Mkuu Ndg Mohammed Issa Simbano na Mkuu wa kitengo cha Tehama ndg Moses Lukoo.

Kesho tarehe 8/8/2021 kutakua na mkutano mwingine katika Jiji la Mwanza ndani ya ukumbi wa Rock City Mall, huku ajenda zikiwa ni zile zile na Uongozi mzima wa JATU PLC utakuwepo ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Ndg Peter Isare Gasaya. Unaweza kufuatilia mkutano huu kupitia youtube channel yetu ya Jatu talk tv.