MKUTANO MKUU WA 4 WA WANAHISA JATU PLC

Leo tarehe 18.12.2021 kampuni ya JATU PLC tumefanya mkutano mkuu wa nne wa wanahisa katika ukumbi wa  blue pearl hotel uliopo ubungo plaza.

Mkutano huu ulianza rasmi majira ya saa mbili na nusu ukiongozwa na mwenyekiti wa bodi Eng. Zaipuna Yonah, huku ukihudhuriwa na viongozi wa Jatu plc akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Peter Isare Gasaya, Meneja Mkuu  Ndg. Mohammed Issa Simbano pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha wa  jatu plc Ndg. Aloyce Valentine Mushy.

Meneja mkuu wa Jatu Plc Ndg. Mohammed Issa Simbano alizungumzia masuala ya kuthibitisha akidi pamoja na yatokanayo na Mkutano Mkuu wa 3 wa wanahisa wa Jatu uliofanyika Novemba 4, 2020. Huku Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Peter Isare Gasaya alizungumzia Sera, Kanuni, Gharama za kilimo na mradi wa ufugaji (2021-2022), pia aliwatangazia rasmi wanahisa kuwa wamepata cheti cha kuruhusiwa kufungua ofisi nchini Kenya maeneo ya Nairobi itakayofahamika kama JATU (K) LIMITED pia aligusia kuhusu mradi wa maembe ambao unatazamiwa kufanyika huko mbeleni.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa bodi alipitisha  pendekezo la wanahisa kupokea gawio lao kwa mwaka 2020 ambayo ni shilingi 18.9 kwa hisa moja ambayo baada ya makadirio inakua ni Sh. 19, Wakati huo huo mwenyekiti alipokea maswali ambayo yalikua yanahusiana na agenda zilizoongelewa na kupatiwa majibu bila kusahau mapendekezo kutoka kwa wanahisa.

Hata hivyo Mkutano huu ulikua na agenda zifuatazo; Kupokea wageni, Kuingia kwa meza kuu, maombi, Kufungua kikao, Kuthibitisha Akidi, Kuthibitisha Agenda, Sera Kanuni, Gharama za kilimo na mradi wa ufugaji (2021-2022) , Gawio la hisa mwaka 2020, mapendekezo ya wanahisa pamoja na maamuzi ya kikao kijacho(tarehe na mahali).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s