MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA JATU PLC YAFANYIKA JIJINI DODOMA tarehe 23.10.2021.

Kampuni ya JATU PLC ambayo tunajihusisha na Kilimo, Viwanda, Masoko pamoja na Mikopo ya kilimo isiyokua na riba, siku ya tarehe 23.10.2021 katika Jiji la Dodoma ndani ya ukumbi wa Mwl. Nyerere, Morena Hotel tulifanikiwa kufanya sherehe ya kihistoria ya Maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kampuni pendwa ya JATU PLC ambapo maadhimisho haya yalihudhuriwa na wageni wa heshima mbalimbali akiwepo Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mh. Jenista Mhagama Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Vijana, Bunge, Ajira na wenye ulemavu. Ndg. Reveliani Ngaiza, Mratibu wa mkakati wa vijana katika kilimo, Mhe. Mwanahamisi Mwankunda Mkuu wa Wilaya ya Bahi pamoja na Afisa mtendaji wa CMSA Ndugu Nicodemus Mkama.

Wageni hao wa heshima walipata nafasi ya kuongea katika maadhimisho hayo ya miaka mitano ya Jatu Plc, ambapo Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda aliwapa moyo uongozi wa JATU PLC na kushangazwa na mwendo mzuri uliopo katika kampuni kwa kufanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi huku Mh. Jenista Mhagama akiahidi kuzitatua haraka changamoto zilizotajwa na Katibu Mkuu Ndugu Mohammed Issa Simbano kwa kupitia tena sera zote zilizotungwa na kuangalia mahali ambapo panatakiwa kufanyiwa marekebisho ya haraka.

Maadhimisho hayo yaliambatana na utoaji wa tuzo, ambapo CEO wa CMSA Ndugu Nicodemus Mkama, Bi Maria Mrutu, mwanachama wa kwanza kabisa kujiunga na JATU, Mrisho Mpoto ambae ni balozi mwekezaji wa JATU, Charles Mwita Gichongo ambae ni muasisi wa JATU, Mosses Lukoo Mkuu wa idara ya Tehama JATU PLC. wote hao walipokea tuzo ambazo walikabidhiwa na Mgeni wa heshima Mh. Jenista Mhagama.


Pamoja na hayo tuliweza kuzindua wa miradi mipya ndani ya JATU PLC ambayo ilizinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa JATU Ndugu Peter Isare Gasaya, miradi hyo ni mradi wa ufugaji, kampuni ya bima pamoja na Bank kwa ajili ya huduma mbalimbali za kifedha. Maadhimisho haya yalisindikizwa na burudani kutoka kwa mabalozi wetu akiwepo Saida Karoli, Barnaba Classic, Linah Sanga na wengine wengi.

Kama ulipitwa na tukio la uzinduzi huu unaweza kutembelea youtube channel yetu www.youtube.com/jatutalk tv kwa ajili ya kujionea tukio zima.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s