Jatu Plc kupitia kampeni ya WIKI YA MAVUNO, ANZA NA EKARI MOJA bado tunaendelea kuhakikisha wakazi wa Kanda ya Kaskazini wanaendelea kunufaika na fursa zilizopo ndani ya Jatu plc, siku ya jana ilikua ndio kilele cha kampeni hii ndani ya mkoa wa Arusha ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa na kuacha alama chanya kwa wakazi wa Arusha, wengi walijiunga na Jatu kwa kuanza na Ekari moja pia kuahidi kuwa watakuwa mabalozi wazuri wa kampuni ya Jatu.
Jatu Plc bado tunaendelea na kampeni hii Kanda ya Kaskazini. Kilimanjaro ndio mkoa unaofuata ambapo maonyesho haya yataanza rasmi tarehe 13.09.2021 mpaka 19.09.2021 timu nzima ya Mpoto Band ikiongozwa na Mrisho Mpoto maarufu kama “Mjomba” watakuwepo kutoa burudani na kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa wanakilimanjaro kwa njia ya sanaa lakini pia meneja mkuu wa Jatu Plc Bw. Mohammed Issa Simbano atakuwepo kuhakikisha kutoa darasa lenye kuwaelimisha wakazi wa kaskazini kuhusu kilimo chenye tija kinachofanyika ndani ya Jatu Plc kwa kuanza na ekari moja.
Usisahau kutembelea YouTube channel ya JATU TALK TV pamoja na Instagram jatu_plc ili kupata taarifa zaidi.


Nawezaje kuanza na heka moja? Namna ya kujiunga na gharama zake pamoja na gharama za hiyo heka moja
LikeLike
Karibu, kwa maelezo kuhusu namna ya kuwekeza na Jatu Plc tafadhali fika katika ofisi zetu zilizopo Posta, Mtaa wa Samora jengo la PSSSF House, Ghorofa ya 6 au wasiliana nasi kwa simu no. 0758396767
LikeLike
Kilimanjaro kampeni ya “Anza na Ekari Moja” itafanyika uwanja gani Ili tuwaelekeze ndugu zetu wahudhurie?
LikeLike
tutakuwepo viwanja vya uhuru pack,karibuni sana
LikeLike