KUELEKEA KATIKA MKUTANO MKUU WA WAKULIMA 2021

Kampuni ya JATU PLC inayo furaha kuwakaribisha wanachama wake katika mkutano mkuu wa wakulima utakaofanyika tarehe 7/8/2021, jumamosi hii jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel na tarehe 8/8/2021 jumapili katika Jiji la Mwanza, ukumbi wa Rock City Mall, Agenda zitakazokuwepo ni pamoja na Ufunguzi wa mkutano, matokeo ya mavuno mwaka 2020/2021, uzinduzi wa miradi mipya, mwenendo wa Hisa za Jatu, na mengineyo.

Mikutano hii inatarajiwa kuongozwa na Mkurugenzi wa JATU PLC Ndugu Peter Isare Gasaya, Kiingilio katika mkutano huu ni risiti ya kununua ama kukodi mashamba na risiti ya manunuzi ya hisa.

Tunaendelea kuwahakikishia wanachama wote watakaohudhuria mkutano huu kuhusu usalama wa afya zenu, kampuni itachukua tahadhari zote kwa kuhakikisha kuwa kila mhudhuriaji atatakiwa kuvaa barakoa, lakini pia kukaa kwa umbali unaoshauriwa na watalaamu wa afya bila kusahau vitakasa mikono. Milango ya ukumbi itafunguliwa rasmi saa 2:00 Asubuhi.

NYOTE MNAKARIBISHWA………!

2 thoughts on “KUELEKEA KATIKA MKUTANO MKUU WA WAKULIMA 2021

  1. Tunashukuru kwa ukaribisho wa Mkutano wa Wana Hisa wa JATU. Kwakweli najivunia kuwepo JATU kama mwanachama mwanzilishi. Kwani najua tulikotoka na JATU na hapa tulipo ni jambo la kumshukuru Mungu Sana. Sikutegemea haya matunda ninayoyapata leo JATU kama ningeyapata.!! Yatosha tu kusema Ahsante Mungu, Ahsante Isare, Simbano, Foime na Mosses. Mungu awabariki Sana.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s