KILELE CHA BUKU TANO INATOSHA

Kampeni ya BUKU TANO INATOSHA ambayo ilianzishwa na kampuni ya JATU ikiwa na lengo la kuuza hisa zake za awali (IPO) kwa bei ya chini ambapo hisa moja ilikua inauzwa shilingi mia tano na kwa elfu tano(BUKU TANO) unajipatia hisa 10 na kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni ya JATU. Uuzwaji wa hisa hizi kwa bei ya ofa ulianza rasmi tarehe 1 Juni 2021 mpaka leo hisa hizi ndo zinafikia katika kilele chake ambapo tumetumia takribani siku 45,kampeni hizi zilifanyika kwa njia tofauti tofauti ikiwepo BAR TO BAR kampeni,Mtaa kwa Mtaa kampeni,kampeni kupitia redio na vipindi mbali mbali vya runinga na mitandao ya kijamii,lakini pia kupitia matawi yote ya ofisi za JATU, matawi yote ya ofisi za NMB, DCB bank, DSE hisa kiganjani huku kote ulikua unaweza kujipatia hisa za JATU.

Kampeni hizi zimefikia tamati leo katika viwanja vya sabasaba(maegesho ya magari) huku zikijumuisha burudani mbalimbali kama sarakasi, singeli, vichekesho, mazingaumbwe.Masupastaa mbalimbali pia walikuwepo pamoja na wasanii maarufu kama Kinata Mc, Mzee wa bwax, Sholomwamba, Senator Kilaka, Mrisho Mpoto pamoja na bendi yake.Pia unaweza kutembelea mitandao yetu ya kijamii Jatu_plc pamoja na youtube chaneli yetu ya Jatu talk tv ili kujionea matukio mengi zaidi.

One thought on “KILELE CHA BUKU TANO INATOSHA

  1. Hongereni Sana JATU Team kwa kuiendesha kampeni ya BUKU 5 INATOSHA, kwani imemfikia kila mwananchi. Ambaye hakuweza kuitumia hiyo Offer kwakutojua basi hana Bahati !! JATU Jenga Afya Tokomeza Umasikini !!

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s