RASMI MKURUGENZI ATAMBULISHA MIRADI MIKUBWA TARIME.

Mkurugenzi wa JATU Plc Ndugu Peter Isare Gasaya

Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC Ndg Peter Isare Gasaya rasmi ametambulisha miradi mikubwa miwili wilayani Tarime mkoani Mara, huku akiwasihi raia kuchangamkia fursa iliyopo ndani ya Wilaya yao kipindi hiki cha ununuaji wa hisa za awali kwa umma kwani wamepata bahati ya pekee. Hayo ameyazungumza akiwa katika Mkutano na wakazi wa Tarime katika viwanja vya Muriba wakati akihutubia kama mgeni rasmi mahali hapo

Peter Isare Gasaya

“nawasihi watu wote wa Tarime huu mradi wa Kilimo cha ndizi ni wenu na nitashangaa kama nyie wazawa mkiniangusha tunakwenda kutatua changamoto ya soko na kulima kitaalamu pia kutoa ajira hivyo nawaomba mshiriki kwenye huu mradi ipasavyo na mnunue hisa sasa ili mpate vigezo na kunufaika zaidi na fursa zilizopo kwenye kampuni yetu”

Wakati huo huo Mkurugenzi ametambulisha Mradi wa Dagaa ambapo wakina Mama wajasiriamali kupatiwa mitaji na kufaidika hasa wale wa halmashauri ya Tarime vijijini huku siku za kununua hisa mtaa kwa mtaa zikifikia kikomo mnamo Julai 15

Lakini pia Meneja masoko JATU PLC amefurahishwa na idadi ya watu waliojitokeza kwenye mkutano huo na kuwasihi wakazi wa Tarime wachangamkie fursa kununua hisa kipindi hiki kifupi Kilichobaki

Hata hivyo Diwani wa kata ya Muriba, eneo ambalo mkutano huo ulipofanyika Ndg Mriko Msami Mariba amefurahishwa na uwepo wa JATU PLC kwenye kata yake na amemuahidi Mkurugenzi kuwa hatamuangusha na atakua balozi mzuri wa kampuni hiyo

Aidha, Mkutano huo ulikua na lengo la kutoa elimu kuhusu uwekezaji na kuutambulisha mradi wa Kilimo cha Ndizi ambacho kinaenda kutatua changamoto za soko kwa wakulima, hayo yanaenda sambamba na uwepo wa kiwanda cha kuchakata ndizi huko Nyanungu na kiwanda ambacho kinatarajiwa kutoa bidhaa mbalimbali,burudani pia zilikuwepo katika mkutano huo ambapo wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo mkongwe Saida Karoli, Enock Bella, Recho bila kusahau wachekeshaji wakali kama Mkaliwenu, Masantula, Ringo na wengine wengi.Jatu talk tv pia wamefanya mahojiano na wakazi wa Tarime ambapo waliongelea zaidi kuhusu ujio wa JATU PLC na fursa hyo katika kijiji chao,unaweza kuyafuatilia mahojiano hayo katika youtube chaneli yetu JATU TALK TV

One thought on “RASMI MKURUGENZI ATAMBULISHA MIRADI MIKUBWA TARIME.

  1. JATU hoyeee !! JATU inazidi kupaaa !! Hongera Sana Mkurugenzi wa JATU Peter Isare kwa juhudi zako za kuwasogezea Huduma ndugu zako !! “Ibada njema huanzia nyumbani”

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s