BALOZI WA NAMIBIA NCHINI (LEBBIUS TANGENI TOBIAS) ATEMBELEA BANDA LA JATU PLC

Leo ni siku ya tano tangu maonyesho ya sabasaba yameanza, huku muamko ukiwa ni mkubwa sana kwa jamii wakizidi kutembelea banda la JATU wakipata elimu zaidi kuhusu HISA pamoja na masuala mazima ya kilimo.

Leo hii banda la JATU lilipata bahati ya kutembelewa na balozi wa Namibia nchini Tanzania mheshimiwa Lebbius Tangeni Tobias na kupokelewa na mwenyeji wake Meneja mkuu wa JATU PLC bwana Mohammed Simbano, ambapo balozi alipata fursa ya kupita katika banda letu lakini pia alipata wasaa wa kujifunza zaidi kuhusu JATU PLC na fursa zilizopo ndani ya kampuni.

Baada ya maongezi haya balozi Lebbius Tangeni Tobias aliwapongeza sana waanzilishi wa JATU na kusema kwamba waliona mbali zaidi na kuwapongeza kwa kutoa fursa ya ajira kwa vijana wengi zaidi na kuahidi kuwa atakua balozi mzuri wa JATU nchini Namibia.

Jatu talk TV tulipata nafasi ya kufanya mahojiano na balozi mheshimiwa Lebbius Tangeni Tobias na unaweza kuyaangalia mahojiano haya kupitia youtube channel ya JATU TALK TV.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s