MSIMU WA SABASABA NA FURSA KUTOKA JATU

Leo ni siku ya nne tangu maonyesho ya sabasaba yameanza na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’UCHUMI WA VIWANDA KWA AJIRA NA BIASHARA ENDELEVU’’. Kampuni ya JATU tunapatikana katika banda namba 56 ambapo timu nzima ya maafisa masoko ipo tayari kukuhudumia kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. karibu tukupe elimu Zaidi kuhusu masuala ya HisaKilimoViwandaMasoko na Mikopo.wa JATU PLC  

Lakini kubwa Zaidi tunaendelea kuwafahamisha  wakulima (wanachama) wetu ya kuwa ili kufanya Kilimo ndani ya JATU PLC ni lazima kumiliki hisa za JATU ambapo kwa shilingi elfu tano (BUKU TANO) unapata nafasi ya kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni kwa kununua hisa 10 ambapo mwanachama huyu atalima ekari moja chini ya usimamizi wa JATU PLC, ili kulima ekari 2-9 mwanachama anatakiwa kuwa na hisa 50 za JATU, ekari 10-49 itakubidi kuwa na hisa 200 na kulima ekari 50 itakubidi kuwa na hisa 1000 na Zaidi.

Hisa za JATU bado zinapatikana kwa bei ya ofa ambapo hisa moja ni shilingi mia tano na hisa kumi utazipata kwa shilingi elfu tano, mwisho wa ofa hii ni tarehe 15 July 2021 kama bado hujanunua hisa za JATU karibu katika maonyesho ya sabasaba banda namba 56 ili uweze kununua hisa lakini pia kupitia matawi yote ya NMB bank, DCB bank, ofisi zote za JATU PLC, DSE hisa kigangani na mawakala (brokers)  huko pia unaweza ukanunua hisa za JATU na kujihakikishia uhakika wa kuendelea kufanya Kilimo chini ya usimamizi bora wa JATU PLC.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s