
Kampuni ya JATU inapenda kuwakaribisha wananchi wote katika kipindi hiki cha msimu wa sabasaba katika banda letu namba 56(ofisi za JATU SACCOS). Haya ni maonyesho ya 45 yakiwa na kauli mbiu ya ’’UCHUMI WA VIWANDA KWA AJIRA NA BIASHARA ENDELEVU”. kauli mbiu hii inaendana na shughuli ambazo JATU PLC inazifanya tukiwa tumejikita zaidi katika masuala ya kilimo,viwanda,masoko,mikopo pamoja na hisa. Lakini fursa kubwa zaidi katika maonyesho haya ya sabasaba ndani ya banda la JATU ni suala zima la hisa ambapo kwa BUKU TANO unajipatia hisa 10 za JATU na kuwa sehemu ya umiliki wa kampuni lakini, pia mabalozi wetu mbalimbali watakuwepo hapo kuhakikisha kuwa unapata elimu zaidi kuhusu hisa, bila kusahau ile kampeni ya mnunulie umpendae ikiwa inaendelea na huu ndio msimu nzuri wa kuonyesha kumjali yule umpendae,tunakukaribisha katika banda letu ambapo utakutana na maafisa masoko wetu na watakupa elimu Zaidi kuhusu faida za kununua hisa za JATU.
JATU mmefanya vizuri Maonyesho ya mwaka huu kwakuongeza huduma ya kupata Hisa za JATU kwani mmeturahisishia Sana sisi wateja wenu. Ni rahisi Sana kumuelekeza mtu kuja kupata huduma 77 kuliko Benki wengine huogopa kuingia Benki.
LikeLike
asante sana. Endelea kufurahia huduma za JATU PLC katika msimu wote wa SABASABA 2021.
LikeLike