
Kampuni ya JATU PLC kupitia tawi la Mwanza imezidi kuwafikia wananchi wengi kupitia kampeni ya BUKU TANO INATOSHA ambayo lengo kuu ni kuuza hisa za awali, kampeni hii ilianza rasmi tarehe 5 Juni 2021 ambapo hisa moja ya JATU inauzwa shilingi 500 hii ni ofa ambayo itaisha tarehe 15 julai 2021.
Muitikio umekua ni mkubwa sana kwa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo wananchi wenye kipato cha chini, kati pamoja na cha juu wamekua wakichangamkia fursa hii kwa wingi ambapo kwa BUKU TANO TU unakua sehemu ya umiliki wa kampuni ya JATU.
kampeni hizi zimekua zikiendeshwa kwa njia mbali mbali kama mtaa kwa mtaa, matangazo kupitia mitandao ya kijamii, runinga pamoja na redio . Lengo la kutumia njia mbalimbali ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata fursa na uelewa zaidi kuhusu HISA bila kujali kipato chake wala elimu.
Mpaka hivi sasa kwa upande wa Mwanza kampeni hizi zimepita katika maeneo tofauti kama Buhongwa, Nyegezi, Malimbe, soko kuu, Mlango mmoja, Makoroboi, Mkuyuni na maeneo mengine mengi.