Kampeni za buku tano ambazo zipo chini ya kampuni ya JATU PLC bado zinaendelea zikiwa na dhima kuu ya kuwafikia wananchi wote wenye uwezo wa kumiliki shilingi elfu tano kwa kuhakikisha kuwa wanakua sehemu ya umiliki wa kampuni kwa BUKU TANO TU.
Leo katika Jiji la Dodoma, kampeni hii ilikuwepo katika maeneo ya Chang’ombe, Nkuhungu, Wajenzi pamoja na sehemu za jirani, kampeni hii imekua ikiacha alama chanya katika jamii kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi mwenye kipato cha kati na cha chini anapata uelewa kuhusu hisa na ananunua hisa za JATU ili kunufaika zaidi baadae.
Kampeni hii tayari imeshapita katika maeneo tofauti tofauti Jijini Dodoma, sehemu kama Fourways, Kizota pamoja na Mnadani, na tayari wananchi wameshanufaika na fursa hii kutoka kampuni ya JATU PLC.







