WASHINDI WA SHINDANO LILILOANDALIWA NA CMSA WAFANYA ZIARA JATU PLC

Washindi wa shindano la masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taaisisi za elimu ya juu (CMUHLIC) linaloendeshwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) , wamefanya ziara ya mafunzo katika kampuni ya JATU PLC na kuweza kupata maelezo ya kina kuhusu hisa za JATU, miradi ya kilimo na fursa nyngine zinazopatikana ndani ya kampuni ya JATU.

Pia walipata nafasi ya kutembelea idara mbalimblai za kampuni ikiwemo idara ya Masoko, Uzalishaji, Sheria, Miradi ,Hisa nk. na hivyo kufahamu vizuri namna kampuni  hii inavyoendeshwa.

Washindi hawa wamevutiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya JATU PLC kwa sababu inatoa fursa nyingi za kukuza kipato na kuondoa umaskini kupitia Kilimo, Viwanda na Masoko. Pia ufanisi mzuri wa Hisa za kampuni katika soko la Hisa la Dar es salaaam (DSE).


Washindi hawa wameahidi kuwa mabalozi wazuri wa  Kampuni  ya JATU na masoko ya mitaji kwa kuwashirikisha na kuwafundisha wanavyuo wengine kuhusu miradi ya JATU na uwekezaji katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE).

2 thoughts on “WASHINDI WA SHINDANO LILILOANDALIWA NA CMSA WAFANYA ZIARA JATU PLC

  1. Safi sana kwa kazi nzuri mlioifanya. Moja ya kampuni kukua ni kuitangaza na kufanya kutambulika zaidi.

    Swali langu pindi tunapouza mazao yetu na kupata ujumbe mfupi wa kukamilika kwa malipo yetu, inachukua muda gani mwanachama kupewa fedha zake?

    Muwe na siku nzuri na kazi njema.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s