Masimbani ni kijiji kidogo kinachopatikana katika wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani,kijiji hiki kimebarikiwa uoto wa asili na ardhi yenye rutuba ya kutosha,wakazi wa kijiji hiki wamejikita zaidi katika kilimo cha mihogo,mahindi pamoja na zao la matunda aina ya maembe.
Mnamo Tarehe 10.04.2021 Uongozi wa Jatu Plc ukiongozwa na Meneja Mkuu Bwana Mohammed Issa Simbano pamoja na mwanasheria Bwana Amon Rwiza walifika katika kijiji hicho baada ya kupokea mualiko kutoka kwa viongozi wa kijiji cha Masimbani, na mara baada ya kufika uongozi wa Jatu Plc ulipata nafasi ya kuongea na kamati kuu ya wajumbe wa kijiji na kueleza dhamira yao, pia walipata nafasi ya kuzungumza na wanakijiji kuhusiana na fursa zinazopatikana ndani ya Jatu Plc na kuwaeleza nia ya Jatu kuwekeza katika kilimo cha tunda la embe kijijini hapo.
Baada ya hapo wanakijiji waliridhia na kufurahia juu ya uwekezaji unaotarajiwa kufanywa katika kijiji hicho mara baada ya kupewa faida za mradi huo, faida hizi ni kama zifuatazo wanakijiji kupata uhakika wa masoko, ajira kwa vijana pamoja na maendeleo mengine mengi kutokana na uwekezaji huo mkubwa unaotarajiwa kufanyika kijijini hapo.







jATU kweli mmedhamiria kufanya mageuzi !! Maana hii spidi mliyo nayo si ya kawaida. Yaani ni ” Kata mti panda mti” Kweli Hakuna kama JATU !! Hongereni Sana vijana wangu. Mungu awaongoze ila msimsahau huyu Mungu aliyewapa huu ujasiri wa udhubutu na kuwaongoza hadi hapa mlipofikia na bado anaendelea kuwapa nguvu, maarifa na Afya njema.
LikeLike