Jumamosi hii ya tarehe 10/4/2021 Jatu Plc kanda ya kaskazini imeandaa semina maalum kwa wakazi wa Arusha na mikoa jirani, semina hii inatarajia kuanza majira ya saa tatu asubuhi, nia na madhumuni ya semina hii ni kutoa elimu zaidi kuhusiana na Jatu Plc na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya Jatu kama fursa ya kilimo, viwanda, masoko bila kusahau mikopo lakini pia uwakala pamoja na hisa za Jatu. Hapa wanachama wapya watapata kuuliza maswali na kujibiwa kwa undani zaidi na maafisa masoko wetu.
Lakini pia semina hii itakua ikitoa maelezo yote ama namna ambavyo wanachama wa Jatu Plc watanufaika baada ya kujiunga na JATU, Semina hii itafanyika mkoani Arusha katika ofisi zetu zilizopo jengo la Saidi condo maarufu kama(furniture collection) ghorofa namba 3,muda ni kuanzia saa 3 asubuh, Njoo wewe pamoja na nduguyo mje mfahamu mengi zaidi yaliyopo ndani ya JATU PLC.

Usikubali kupitwa
Njoo ujiunge katika ulimwengu wa fursa
Hakuna kiingilio. Nyote Mnakaribishwa.