Hii ni safari iliyoandaliwa na JATU PLC, ikiwa na lengo la kwenda kutembelea mradi wa parachichi uliopo mkoani Njombe.
Mradi huu upo chini ya usimamizi wa JATU PLC lakini unamilikiwa na wanachama wa JATU PLC, hii itakua ni mara ya kwanza kwa wanachama kwenda kujionea kwa macho maendeleo ya mradi huu, safari hii itakua ni tarehe 23/4/2021 mpaka tarehe 26/4/2021. Gharama za safari ni shilingi 250,000 ikijumuisha malazi, chakula, vinywaji pamoja na shamba boots.
Malipo yanafanywa kupitia mfumo wetu wa JATU MARKET na tunawasihi wanachama kufanya malipo yao mapema kwani nafasi ni chache, lakini pia kutakua na tukio maalum la kuzindua kampuni ya kitalii yaani TRAVEL 301 inayoshirikiana na JATU PLC bila kusahau kivutio cha JATU GREEN GOLD VILLAGE hapa wanachama watapata nafasi ya kujionea kijiji hiki na kupata wasaa wa kupata burudani kama vinywaji pamoja na mziki. JATU PLC inaendelea kuwasihi wanachama wake kuendelea kununua mashamba ya parachichi ambayo yanapatikana kwa shilingi milioni moja kwa ekari ambapo kama utanunua shamba la parachichi mwaka huu yaani 2021 hadi kufikia 2024 mwanachama atakua ameshavuna.
Twenzetu Njombe
Wekeza na JATU PLC katika kilimo cha parachichi 2021
JATU Ile pesa ambayo mkulima anatakiwa aitafute anaionesha vipi kwenu, namaanisha ninyi mathibitishaje?
LikeLike
tafadhali wasiliana nasi kwa simu namba 0758396767 kwa maelekezo zaidi. Asante
LikeLike
Kiasi ambacho mkulima anatakiwa kuwa nacho kabla hajapata mkopo kitatunzwa wapi na maanisha mkepeshaji atakithibitishaje?
LikeLike
habari, akiba za mazao, binafsi na za kila mwezi zote huwekwa kwenye akaunti za benki za JATU SACCOS, tafadhali wasiliana nasi kwa simu namba 0765002660 kwa maelezo zaidi. Asante
LikeLike
Hello habari kwanza hongereni sana kwa mradi huu wa parachichi. Swali langu je kwa sisi tuliochelewa kupata taarifu kunautaratibugani tukitaka tuwekeze kwenye kilimo hicho cha parachichi chini ya SACCOS yenu
LikeLike
Habari Gift, tafadhali wasiliana na kitengo cha JATU SACCOS kwa namba hizi 0765002660 kwa maelekezo zaidi, asante.
LikeLike