UZINDUZI WA SERA ZA KILIMO

Ikiwa ni mkutano wa kwanza tangu kuingia mwaka 2021, kampuni ya JATU PLC mapema siku ya Jumamosi ya tarehe 27 Februari 2021 ilifanya Uzinduzi wa Sera za Kilimo katika ukumbi wa Blue Pearl ikijumuisha wanachama kwa wasio wanachama wa JATU.

Akizungumza na washiriki wa Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC Ndg. Peter Isare alisema kuwa, “sera hizi mpya zinalenga kuiwezesha kampuni kukua kwa kasi kwa kuongeza ufanisi kwa kutekeleza na kuboresha miradi mipya ya kilimo inayotarajiwa kuanzishwa. Hii ni kutokana na gawio la 25% la faida itakayotokana na usimamizi wa shamba ambayo itatolewa kwa kampuni kama gharama ya usimamizi wa shamba la mwanachama.
Aliongeza, “kwa kupitia sera hii tunaamini kwamba watu wenye mawazo ya kibunifu wataweza kunufaika kupitia ushiriki wao kwenye kwenye miradi ya kilimo kwa kupata gawio la asilimia 25% kutokana na mawazo yao ya kibunifu yaliyobadilishwa na kuwa katika miradi inayoonekana hivyo kampuni pia kunufaika na miradi ya kilimo kuongezeka”.

Aidha Ndg. Peter Isare alizungumzia juu ya sifa na vigezo vya namna mmoja anaweza kushiriki katika miradi ya JATU ya kilimo kikamilifu ikiwa ni Pamoja na; kumiliki hisa za kampuni zilizoorodheshwa mwishoni mwaka jana katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), kukubali kutumia mfumo wa masoko wa JATU market app kwa kununua bidhaa zinazozalishwa na JATU kila mwezi ili kujihakikishia  kupata gawio la faida kila mwisho wa mwezi na mwisho kufikia adhma ya kampuni ya Kujenga Afya na Kutokomeza Umaskini kwa kutumia bidhaa bora za JATU zinazozingatia afya ya mlaji wake. Vilevile Ndg. Isare alitoa rai wa washiriki wa mkutano huo kuitumia fursa ya JATU SACCOS kwa kujiunga na chama hiko na kuanza kuweka akiba mapema ili kuweza kutimiza vigezo na kuweza kunufaika na mikopo ya kilimo isiyo na riba kwa masharti nafuu.

One thought on “UZINDUZI WA SERA ZA KILIMO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s