TAARIFA KUHUSU MIRADI YA JATU PLC ILIPOFIKIA.

JATU PLC ni kampuni ya umma ambayo imejikita katika shughuli za kilimo,viwanda na masoko. Kampuni pia hutoa mikopo isiyokua na riba kwa wanachama wakulima, ambayo hurudishwa mara tuu baada ya mavuno,  pia na mikopo ya maendeleo yenye riba nafuu kwa wanachama kupitia JATU SACCOS LIMITED. Mfumo wa kilimo ambao kampuni huendesha ni kilimo shirikishi ambapo wakulima ambao ni wanachama wa JATU PLC hulima kwa pamoja na mara baada ya mavuno basi kila mwanachama hupatiwa mavuno yake kutokana na hekari alizolima, kilimo hicho shirikishi kimekuwa ni chachu kwa wakulima kwa kuwa kimekuwa kikiwabeba wakulima kwa kupata idadi karibia na ile iliyokadiriwa.

Mazao yote yanayolimwa na JATU PLC huuzwa kupitia mfumo wa JATU MARKET, na kampuni ndio mteja pekee wa mazao hayo.  Kupitia mazao haya ambayo hutumika kama malighafi katika viwanda vya kampuni, bidhaa mbali mbali huzalishwa kutokana na mazao hayo na kuuzwa kwa wanachama wa JATU kupitia mfumo wa JATU MARKET. Bidhaa hizi pia hupatikana katika maduka makubwa ambayo yanamilikiwa na kampuni maarufu kama JATU SUPERMARKET na pia kupitia mawakala wa JATU ambao wanapatikana Tanzania nzima. Hizi bidhaa huuzwa katika mfumo wa soko la mtandao (Network Market) ambao mwanachama anaweza kutengeneza mtandao wake wa walaji na kujipatia gawio la faida kila mwisho wa mwezi kulingana na manunuzi yake yeye na pamoja vizazi vyake.

MRADI WA MPUNGA MBINGU MKOANI  MOROGORO.

Katika mkoa wa Morogoro wilayani Mbingu JATU Plc wamejikita katika kilimo cha mpunga, ambapo JATU PLC inamiliki mashamba makubwa ya mpunga, baada ya mpunga kuvunwa huchakatwa katika kiwanda cha kampuni ,na kufungashwa katika vifungashio maalum vyenye nembo ya JATU, na bidhaa hizi huwekwa sokoni ambapo wanunuzi  wakuu wa bidhaa hizi ni wanachama wa JATU wenyewe.Kwasasa hatua iliyofikia ni upandaji na kupiga haro,zoezi hili

linategemea kuendelea kufanyika mpaka mwezi wa kwanza katikati ili kumaliza zoezi hilo la uandaaji wa mashamba.

MRADI WA VIAZI LISHE RUVUMA

Viazi lishe ni mradi unaofanyika mkoani Ruvuma wilaya ya Madaba chini ya usimamizi wa JATU PLC ambapo mradi huu wa viazi lishe unatarajiwa kuanza rasmi baada ya maandalizi ya mashamba kukamilika kusafishwa, na kupiga haro. Tayari kazi ya kusafisha mashamba ikiwemo kung’oa visiki na kuondoa majani na uchafu mwingine shambani umeshaanza kufanyika. Idara ya Miradi na Utafiti inaeleza kuwa mpaka sasa zoezi la kusafisha mashamba limekamilika kwa 60% na pia shughuli nyingine inayoendelea ni kuunganisha miundombinu ya barabara na madaraja kutokea Songea kuelekea Dar es salaam ambapo zoezi hili mpaka sasa limekamilika kwa 70%

MRADI WA PARACHICHI NJOMBE.

Kilimo cha parachichi ni mradi mpya kwa mwaka huu wa 2021 ambao utakua unafanyika mkoani Njombe katika kijiji cha Taweta chini ya usimamizi wa JATU PLC, mpaka sasa kinachoendelea ni maandalizi ya mashamba ambayo yamekwishaanza kufanyika, ukubwa wa shamba ni takriban ekari 1,000 na mpaka sasa ekari 400 zimekwisha safishwa tayari kwa kuanza zoezi la kuchimba mashimo kwa ajili ya kuhamishia miche shambani kipindi cha mwezi february 2021. Zoezi la ukaguzi wa mipaka na kuweka alama katika shamba hilo limefanyika kwa umahiri mkubwa na zoezi la kujenga eneo la kuhifadhia miche kwa lengo la kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa fangasi za mizizi kutoka kwa mche wenye maambukizi kwenda kwa micheisiyokuwa na maambukizi. Kilimo cha parachichi kinakadiriwa kuchukua muda wa miaka mitatu mpaka kuvunwa kwa parachichi, mradi huu licha ya kuchukua muda mrefu  lakinipia ni mradi wenye faida kubwa tarajiwa baada ya mkulima kuanza kuvuna, lakini pia mkulima atakua na uwezo wa kuvuna kila mwaka baada ya miaka hiyo mitatu

MRADI WA NDIZI TARIME.

JATU iliamua kuanzisha mradi wa ndizi wilayani tarime  kutokana na rutuba ya ardhi ya mkoa wa Mara na wilaya ya Tarime  katika kilimo cha ndizi. Siku ya tarehe 29/12/2020, maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ndizi yalikamilika na wanakijiji hususani wakulima wa zao la ndizi, Viongozi wa serikali akiwemo Diwani kata ya Nyanungu alihudhuria. Uzinduzi wa mradi huu kwa ujumla ulileta muamko mkubwa kwa wakulima na wananchi wa kata ya Nyanungu kwa ujumla kwani ulileta matumaini ya maendeleo ambayo yamekua yakisubiriwa kwa muda mrefu. Kwa sasa wananchi hao wanatumaini la kulima kisasa zaidi na kupata soko la mazao yao baada ya mavuno na vilevile ongezeko la ajira hususani kwa wanawake na watu wote ambao wataonyesha nidhamu na jitihada katika kujituma kufanya kazi.

MRADI WA MAHINDI KITETO.

Wilaya ya kiteto mkoani Manyara kampuni ya Jatu plc  imewekeza katika kilimo cha mahindi na alizeti. Maendeleo ya mradi kwa sasa  yamefikia kwenye upandaji  na kuna mahindi ambayo yamekwisha chipua na kuota na zoezi hili la kupanda shamba linategemea kukamilika mnamo mwezi wa pili mwaka huu. Ikumbukwe kwamba shamba hili linapandwa kisasa kabisa kwa kutumia trekta ambalo hulima shamba. Eneo kubwa la shamba tayari limekwisha andaliwa tayari kwa kuendelea na zoezi la kupanda. Tuliweza kuzungumza na mkuu wa Idara ya Miradi na Utafiti ambae alizungumzia maendeleo ya mradi na kuelezea shughuli zinazoendelea kwa sasa ni upigaji wa dawa kwa ajili ya kuua magugu ambayo yameota katika shamba, shughuli za kupanda pia zinaendelea sambamba na usafishaji wa maeneo mengine ya shamba.

Imetolewa na

Jatu Public Limited Company

4 thoughts on “TAARIFA KUHUSU MIRADI YA JATU PLC ILIPOFIKIA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s