Mapema siku ya jana, tarehe 29.12.2020 kampuni ya JATU PLC ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Peter Isare Gasaya imezindua rasmi mradi wa kilimo cha ndizi mkoani Mara wilayani Tarime katika viwanja vya shule ya msingi ya Mangucha.

Katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Peter Isare alieleza kuwa,”Lengo kuu la mradi huu mpya ni pamoja na kuwawezesha vijana kupata ajira ya kudumu kupitia kilimo cha ndizi lakini pia kuwasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa masoko ya zao hilo la ndizi”. Aliendelea kusema,”mradi huu kwa kuanza utahusisha wakazi wa wilaya ya Tarime vijijini ambao watatarajia kupata mafunzo ya kitaalamu ya kutosha kutoka kwa wataalamu wa masuala ya kilimo ili kufanya kilimo chenye tija kwa matokeo chanya”.
Aidha alisisitiza watu wajitokeze na kujiunga kwa vikundi kwa wingi ili kuweza kunufaika na mradi huu kwa kupata mafunzo na usimamizi wa kisasa na wa kitaalamu katika mashamba yao, kunufaika na mikopo ya kilimo isiyokuwa na riba, uhakika wa masoko kwa mazao yao lakini pia ajira za kudumu kwa wakazi wa maeneo ya mradi huu. Halikadhalika kujenga miundo mbinu kama vile visima na mashine ili kupata maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji na maendeleo mengine ya kijamii kama ujenzi wa barabara katika vijiji husika, nk.






Hongera Sana Mkurugenzi wa JATU PLC. kijana Peter Isare kwa juhudi zako za kuwapatia vijana wetu ajira kwakupitia miradi mbalimbali hapa Tanzania. Mungu akuongoze ktk kutimiza ndoto zako. Inshaallah.
LikeLike