RIPOTI YA MWENENDO WA HISA ZA JATU PLC KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

TAREHE 11 December, 2020

Leo ni takribani siku ya 18 tangu JATU PLC irodheshe hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) Mnamo tarehe 23 November, 2020.

Kampuni iliingia sokoni na kuorodhesha vipande 2,164,349 vya hisa kwa bei ya Tshs. 420 kwa hisa moja.

Siku ya leo tumefungua soko kwa bei ya Tsh 820 na ubaoni kulikua na jumla ya hisa zinazosubiri kununuliwa kutoka siku ya jumanne. Jumla ya hisa zilizoweza kuuzwa na kununuliwa leo ni hisa 2910 katika miamala 10 kwa bei tofauti tofauti ya Tsh 840, 860 na 900 ambayo imepelekea kua na bei ya wastani wa soko ya Tsh 865 ambayo tumefungia soko siku ya leo.

Bei ya hisa imeongezeka kwa kiasi cha asilimia 4.88% kutoka 820 mpaka 860 na Jumla ya thamani ya hisa zilizouzwa siku ya leo ni Tsh 2,512,400. Na Idadi ya ofa zilizobaki zikisubiri kununuliwa ni hisa 12,672. Pia kwa siku ya leo tumefunga soko kukiwa naoutstanding offers (wanaosubiri kuuza )ni hisa 5.

Thamani ya kampuni imezidi kuongezeka mpaka kufikia billion 1.86 ukilinganisha na bilion 1.08 ya tarehe 23 November, 2020.

Uongozi wa JATU PLC unaendelea kuboresha huduma zake na kupanua uwekezaji katika kilimo, viwanda na masoko ili kuhakikisha wanahisa wake wananufaika kutokana na uwekezaji wao wanaoendelea kufanya na JATU.

Kwa sasa tunawashauri wakulima na wote wenye hisa kuwekeza katika mradi wa kilimo cha parachichi unaosimamiwa na JATU katika mkoa wa Njombe. Mradi huu unafaida kubwa sana na ya muda mrefu na ukizingatia soko lake ni la uhakika kitaifa na kimataifa.

Tembelea app ya JATU MARKET inayopatikana Playstore na AppStore uweke oda yako sasa kwa manufaa ya kiuchumi Leo na kesho.

Pia tunaendelea kukukaribisha ufike katika ofisi zetu zilizo Karibu na wewe nchi nzima ili uweze kujaza fomu ya uwakala uwe wakala wa huduma na bidhaa za jatu.

Lakini pia endelea kula bidhaa za JATU ili mwisho wa mwezi upate gawio la faida, mjulishe na mwenzako kuhusu huduma za jatu na wewe utapata commission kwa kutoa tu taarifa kwa mwenzako na akajiunga na kutumia huduma za jatu kupitia app ya JATU MARKET na Jatu Pesa.

Imetolewa na,
Sarafina Adrian
Mchumi na mchambuzi wa soko la hisa ,JATU PLC
11.12.2020

5 thoughts on “RIPOTI YA MWENENDO WA HISA ZA JATU PLC KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

  1. Hello! Nahitaji kununua share kwenye kampuni ya Jatu but I don’t know how to do so.I am so please if you can assist me.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s