HATIMAYE JATU PLC KUINGIA KATIKA SOKO LA HISA (DSE).

Ikiwa ni mwaka wa nne tangu kuanzishwa kwa kampuni ya JATU PLC, mnamo tarehe 14.11.2020 kampuni ya JATU PLC iliitisha mkutano mkubwa katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, iliyokutanisha bodi ya wakurugenzi wa JATU PLC pamoja na wanachama wa kampuni. Ajenda kuu ikiwa ni mchakato wa kampuni ya JATU PLC kuingia katika soko la HISA. Aidha ajenda mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo, ikiwemo uwasilishaji wa ripoti ya mwaka na taarifa za fedha, kupitisha na kuzindua miradi mipya ya kilimo kwa mazao ya mboga mboga, kitunguu na viazi lishe pamoja na kuzindua fursa ya uwakala wa bidhaa za Jatu

Mkurugenzi wa JATU PLC Ndg. Peter Isare Gasaya ameshauri watanzania kutambua fursa zitolewazo na kampuni sambamba na kujiunga ili kuweza kushiriki katika fursa na miradi mbalimbali inayoendeshwa na kampuni kupitia umiliki wa hisa za kampuni. Aidha aliendelea kueleza kuwa baada ya kuingia katika soko la hisa kuanzia mwaka huu 2020 kampuni inategemea mahitaji makubwa ya bidhaa kuongezeka, wawekezaji hususani kwenye miradi ya kilimo kuongezeka na hivyo kufikia dhima ya kampuni ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora katika ukanda wa Afrika Mashariki sambamba nakutokomeza umasikini.

Aliendelea, “Kilimo kwa tafsiri ya JATU ndio nguzo na mustakabali wa kujenga kampuni ya JATU kwa kupitia matokeo ya mwisho ya kufanikisha ‘KULA ULIPWE’. tukifanikiwa kuwa na mazao mengi, viwanda na bidhaa na uwepo wa mawakala wengi tutahakikisha ufikiaji wa bidhaa za JATU kwa kila mtu”. Pia Ndg. Peter Isare aliwataka watanzania kuona fursa katika kilimo cha zao la parachichi ili kunufaika na soko la kimataifa.

Naye Mwenyekiti wa bodi wa JATU PLC Mhandisi Dk.Zaipuna Yona alisisitiza na kutoa wito kwa vijana kuondokana na fikra za kudhani ni wazee ndio wanatakiwa kujihusisha na masuala ya uwekezaji katika masoko ya hisa na kuwataka wajifunze zaidi katika faida za uwekezaji kupitia masoko ya hisa. Aidha Dk. Zaipuna aliendelea kuelezea faida mbalimbali za kujiunga na kampuni ya JATU PLC zikiwemo kupata usimamizi wa kitaalamu katika shughuli za kilimo, uwezeshwaji wa mikopo isiyo na riba, faida ya kupata gawio la faida kutokana na manunuzi ya bidhaa za chakula zinazouzwa na kampuni ya JATU. nk.

4 thoughts on “HATIMAYE JATU PLC KUINGIA KATIKA SOKO LA HISA (DSE).

  1. Hongereni Sana Jatu kwa hatua hii, Mimi kama mkulima mpya natarajia mafanikio makubbwa tukiwa pamoja. Tunazidi sambaza taarifa ili Watanzania wengi wanufaike kwa kujiunga na Jatu.

    Like

    1. habari, tafadhali pakua app ya JATU inayopatikana playstore/appstore kisha jisajili n baada ya kukamilisha usajili na kufanya malipo ya kiingilio tsh 30,000/= utapokea ujumb kutoka JATU wenye namba yako ya uanachama pamoja na neno lako la siri, taarifa ambazo utakua ukizitumia kuingia kwenye app ya JATU na kupata taarifa mbalimbali. KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0758396767, ASANTE

      Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s