Ikiwa zimebaki siku chache, kampuni ya JATU PLC inapenda kuwataarifu wanachama wa JATU na wote ambao bado hawajajisajili kuwa wanachama juu ya mkutano mkubwa wa wanahisa unaotarajia kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 14.11.2020.
WALENGWA
- Wanahisa wa JATU PLC.
- Wanachama wa JATU.
- Wageni ambao si wanachama wa JATU na wangependa kufahamu fursa zinazopatikana ndani ya JATU.
AJENDA
- Mrejesho kuhusu mchakato wa kampuni kuingia katika soko la hisa.
- Uzinduzi wa fursa ya Uwakala wa uuzaji na usambazaji wa bidhaa za JATU.
- Uzinduzi wa miradi mipya ya kilimo kwa mazao ya VIAZI LISHE na VITUNGUU.
JINSI YA KUSHIRIKI
- Washiriki wote wanaotarajia kushiriki katika mkutano huu wanatakiwa kuwa na fulana – (T-shirt) ya JATU inayopatikana katika mfumo wa JATU MARKET au kwa kufika katika ofisi za Makao Makuu ya JATU zilizoko Posta, mtaa wa Samora katika jengo la PSSSF HOUSE ghorofa namba 6.
MUDA
- Kuanzia saa 02:00 Asubuh mpaka 11:00 Jioni
JATU NI YA KWETU
WOTE MNAKARIBISHWA
