NANENANE NA JATU TALK YAACHA ALAMA KWA WADAU WA KILIMO NCHINI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Historia yaandikwa siku ya wakulima Nanenane na Jatu Talk iliofanyika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza ambapo kulifanyika mazungumzo ya wakulima, wadau wa kilimo na kampuni ya JATU ambapo mgeni rasmi alikua Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo akiwakilishwa na Mratibu wa mkakati wa vijana kushiriki kilimo Mh. Revelian Ngaiza. Mazungumzo hayo yalioambatana na mrejesho wa mavuno ya kilimo msimu wa 2019/20 na burudani mbalimbali kutoka kwa balozi wa Jatu msanii Mrisho Mpoto yalikua ya aina yake na kuacha gumzo kwa wakazi wa Dar es salaam na mikoa ya karibu.

Mazungumzo hayo ambayo yalihusisha wakulima zaidi ya mia saba yamefanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na muitikio wa wadau wa kilimo ambao wamevutiwa na fursa za uwekezaji kupitia kilimo cha JATU hasa mradi mpya wa kilimo cha parachichi ambao ulikua kivutio kikubwa kwa wawekezaji. Lengo la JATU ni kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo nchini huku pia kubadilisha maisha ya wakulima kutoka kwenye dimbwi la umasikini kwa kukifanya kilimo kuwa biashara isio na wasiwasi hivyo kampuni huanza kwa kufanya utafiti wa mashamba, usimamizi wa kilimo, hutumia pembejeo za kisasa, mikopo ya kilimo isio na riba pamoja na masoko ya uhakika ya mazao na bidhaa zitokenazo na kilimo.

Meneja Mkuu wa JATU Mr. Issa Mohamed Simbano alitoa mrejesho wa mavuno kwa wakulima walioshiriki kilimo msimu wa 2019/2020 ambapo wakulima wengi walipokea ripoti hizo kwa bashasha kwani walifikia malengo kwa asilimia kubwa. Pia Mkurugenzi Mtendaji wa JATU Mr. Peter Isare aliahidi kuwa kampuni itaendelea kushirikiana na wadau wenye mawazo mazuri ya kilimo kupitia mfumo mpya wa Jatu talk ambao umelenga kukutanisha wabunifu wa mawazo na wenye mitaji ya kuwekeza huku akitolea mfano wa mwanachama wa JATU Irene Mangoli ambae ndie alieleta wazo la kilimo cha parachichi na JATU kuliwezesha kufanikiwa.

Wageni waalikwa kutoka SAGCOT na TIB waliahidi kuendelea kushirikiana na JATU ili kuongeza chachu ya maendeleo ya kilimo nchini kwani JATU imeonesha mfano mkubwa kwa kubadilisha mtazamo wa wakulima nchini kutoka kilimo cha mazoea na kuelekea kilimo cha kisasa cha kibiashara zaidi.

JATU ~ Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s