NANENANE NA JATU 2020, USIKOSE KUTEMBELEA MABANDA YETU

Nanenane ni sikukuu ya wakulima ambayo huazimishwa nchini kote kila tarehe 08 ya mwezi wa nane yenye lengo la kuhamasisha mchango wa wakulima kwenye uchumi wa taifa. Sherehe hizi huandaliwa na kuratibiwa na wizara ya kilimo, chakula na ushirika kwa kushirikiana na shirika la chama cha kilimo Tanzania(TASO). Maonesho haya huhusisha taasisi, wizara na mtu mmoja mmoja anaeshughulika na kilimo.

Miaka iliyopita sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa. Maadhimisho haya husherehekewa katika ngazi ya kanda ambapo kanda ya nyanda za juu za kusini hufanyika viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya. Kwa kanda ya Kaskazini, sherehe hufanyika viwanja vya Themi, Arusha , wakati kanda ya Mashariki hufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Morogoro na Kanda ya Ziwa, hufanyika Mwanza, Viwanja vya Nyamhongolo na Kanda ya mwisho ni kusini, hufanyika Ngongo.

Kilimo ni moja ya sekta muhimu sana kwenye ukuaji wa uchumi kama taifa pia huchangia takribani nusu ya ajira zote nchini. Pia kilimo huchangia karibu theluthi(1/3) ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Tanzania na pia mauzo ya bidhaa nje ya nchi kwa asilimia 85.

Pamoja na umuhimu wake kwa uchumi na maendeleo ya nchi, kilimo bado kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo hupunguza tija kwenye sekta hii. Kama nchi zingine za Kiafrika ambazo hutegemea kilimo kama kichocheo cha uchumi, siku ya Wakulima ni siku ya kuheshimu wakulima na kuzingatia mchango wa sekta hiyo kwa nchi.

Lengo ni kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi kwaajili ya kuongeza tija na uhakika wa chakula, kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko. Maonesho ya nanenane huanza Agosti 1 mpaka Agosti 8 kila mwaka.

Maonesho ya mwaka huu 2020 ambayo ni maonesho ya 28 yenye kauli mbiu isemayo “Kwa maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020” ambayo yanafanyika kitaifa viwanja vya Nyakabindi wilaya ya bariadi mkoa wa Simiyu. Mgeni rasmi siku ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho ni Mh. Samia Suluhu makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atakua mgeni rasmi siku ya kilele cha maadhimisho tarehe 08 mwezi wa nane 2020.

JATU PLC tunashiriki maonesho haya kitaifa mkoani Simiyu banda namba 12 karibia na banda la wizara ya kilimo, kanda ya kaskazini maonesho tunashiriki mkoani Arusha banda la halmashauri ya wilaya ya Kiteto, kanda ya kati tunashiriki mkoani Dodoma Banda la jiji la halmashauri ya jiji Dodoma, na ukanda wa pwani tupo Mkoa wa Morogoro banda la halmashauri ya wilaya ya Temeke .

Tunawakaribisha wadau mbalimbali kutembelea banda letu ili kupata elimu ya fursa ya uwekezaji kupitia huduma zetu za kilimo, viwanda, masoko na mikopo ili kutimiza azma yetu ya kujenga afya na kutokomeza umasikini.

JATU- Jenga Afya Tokomeza Umasikini

One thought on “NANENANE NA JATU 2020, USIKOSE KUTEMBELEA MABANDA YETU

  1. Hongereni Sana Uongozi wa JATU kwakuwawezesha Wakulima wa JATU kushiriki maonyesho ktk Kanda zote nchini Tanzania. Nawapa Big up πŸ‘πŸ‘πŸ‘

    Liked by 1 person

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s