Tunapenda kuwafahamisha wadau wa kilimo, wanachama wakulima na ambao sio wakulima wa Jatu kwamba kutakuwa na kikao cha wakulima wa Jatu mnamo Tarehe 08 Agosti, 2020.
Mkutano huu utakua na agenda zifuatazo;
- Kuingia na kukagua taarifa za wakulima, kila mkulima atakagua faili la taarifa zake za kilimo Jatu.
- Mrejesho wa kilimo kwa msimu wa 2019-2020 zao la Mpunga, Mahindi, Alizeti na maharage. Hapa pia tutazindua njia mpya ya mkulima kuuza mazao yake kirahisi zaidi na kwa faida zaidi.
- Mkakati wa kilimo kwa msimu 2020-2021, zao la mpunga, mahindi, Alizeti, maharage na Machungwa.
- Miradi mipya ya kilimo na Jatu iliyobuniwa mwaka 2020 (Parachichi na viazi lishe).
- Mengineyo
Ukumbi: Kilimanjaro VIP
Hotel: Blue Pearl Hotel
Jengo: Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Ubungo, Shekilango
MGENI MUALIKWA(ATAKUWEPO): MRISHO MPOTO

Gharama za mkutano zipo vipi?
LikeLike
Mkombozi wa wanyonge .endelea kutuinua wakulima wadogo.
LikeLike
Tupo pamoja suitbert, endelea kufurahia huduma za JATU
LikeLike
Asante kwa Taarifa
LikeLike
Habari Boniphace,
Karibu sana usikose kuhudhuria
LikeLike
tunaomba kupata updates za yote yatakayoendelea kwa sisis ambao tutashindwa kufika
LikeLike