USIPITWE NA MKUTANO WA NANENANE NA JATU TALK 2020 UKUMBI WA UBUNGO PLAZA, KWA WAKULIMA NA WADAU WA KILIMO WOTE MNAKARIBISHWA

Habari,

Tunapenda kuwafahamisha wanachama wakulima na ambao sio wakulima wa Jatu kwamba kutakuwa na kikao cha wakulima wa Jatu mnamo Tarehe 08 Agosti, 2020 ili kushiriki mkutano huu unatakiwa kufata maelekezo yalioyoanishwa hapa chini; –

Walengwa:

Wanachama wa jatu wakulima waliolima msimu wa mwaka 2019-2020 na wale wanaotegemea kulima msimu wa mwaka 2020-2021. Pia wageni ambao sio wakulima wa Jatu kwa sasa na wangependa kujua kuhusu kilimo wanaruhusiwa kushiriki na kujionea tukio hili.

Ajenda:

  1. Kuingia na kukagua taarifa za wakulima, kila mkulima atakagua faili la taarifa zake za kilimo Jatu.
  2. Mrejesho wa kilimo kwa msimu wa 2019-2020 zao la Mpunga, Mahindi, Alizeti na maharage. Hapa pia tutazindua njia mpya ya mkulima kuuza mazao yake kirahisi zaidi na kwa faida zaidi.
  3. Mkakati wa kilimo kwa msimu 2020-2021, zao la mpunga, mahindi, Alizeti, maharage na Machungwa.
  4. Miradi mipya ya kilimo na Jatu iliyobuniwa mwaka 2020 (Parachichi na viazi lishe).
  5. Mengineyo

Eneo:

Ukumbi: Kilimanjaro VIP

Hotel: Blue Pearl Hotel

Jengo: Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Ubungo, Shekilango

Muda:

kuanzia saa 02:00 Asubuhi – saa 10:00 Jioni

Huduma zitakazotolewa:

  1. Chai ya asubuhi
  2. Chakula cha mchana (Lunch)
  3. Notebook na kalamu
  4. Kitabu cha Jatu Kilimo 2019 – 2020

Kiingilio:

T-shirt ya Jatu

Kila mtu atakaye shiriki mkutano huu lazima avae T-shirt maalumu ya Jatu ambayo itapatikana siku hiyo mlangoni. Malipo ya T-shirt hizi yatafanyika kupitia Jatu Market App na kila mmoja ataandika size yake hapo kwenye Jatu Market App wakati unatuma oda yako baada ya kuchagua neno ‘‘Pick Up’’ basi kwenye neno la taarifa nyingenezo utasema size ya Tshirt na kulipia Tsh. 20,000/= Lipia T-shirt kabla ya tarehe 03.08.2020 ili kuthibitisha ushiriki wako.


“JATU – Jenga Afya Tokomeza Umaskini”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s