HAKIKI ORODHA YA WAKULIMA WA JATU MSIMU 2020/2021 KWA AMBAO BADO HAMJAKODI, ENDELEA KUKODI AU KUNUNUA MASHAMBA KUPITIA JATU MARKET APP ILI USIKOSE NAFASI MSIMU HUU

DOWNLOAD ORODHA YA WAKULIMA 2020/2021

NDUGU MWEKEZAJI KARIBU ULIME NA JATU PLC BILA STRESS ZOZOTE

This image has an empty alt attribute; its file name is whatsapp-image-2020-04-22-at-1.26.39-pm.jpeg

Katika huduma(fursa) ya kilimo JATU PLC hufanya kilimo shirikishi yaani inashirikiana na wanachama wake kufanya kilimo, kampuni ya JATU PLC husimama kama msimamizi wa miradi yote ya kilimo na wanachama wake(wakulima) kama wawekezaji katika miradi hiyo ya kilimo. Kampuni hutafuta maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania ambayo yanafaa kufanyiwa kilimo na kuyafanyia utafiti wa kina kabla ya kuanza kuyafanyia uwekezaji, kampuni hutumia wataalamu wake wenye uzoefu mkubwa katika kufanya tafiti za maeneo husika ili kubaini aina ya mazao ambayo yanafaa kulimwa katika ardhi husika, hali ya hewa, changamoto katika eneo husika n.k yote haya hufanyika ili kampuni iweze kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija (faida). Baada ya kujiridhisha na tafiti toka kwa wataalamu wetu kampuni uwashirikisha wanachama tafiti hizo na kuzifanyia maamuzi ya utekelezaji.

Mpaka sasa watafiti wetu wamefanya tafiti za mazao matano na tayari wakulima wawekezaji wa kampuni wameanza kuwekeza katika mazao waliyoyachagua na kampuni ya JATU PLC imekuwa msimamizi mkuu wa miradi hiyo yote. Maeneo ambayo yameteuliwa kufanyiwa kilimo ni yafuatayo;

Na.ZaoEneoJumla ya Ekari
1.AlizetiKiteto Manyara5,000
2.MahindiKiteto Manyara5,000
3.MpungaMbingu Morogoro5,000
4.MaharageKilindi Tanga3,000
5.MatundaMuheza Tanga1,000

MCHANGANUO WA UWEKEZAJI KATIKA MAZAO YANAYOLIMWA NA JATU PLC

1.Alizeti

This image has an empty alt attribute; its file name is artboard-1.png

Alizeti ni zao muhimu katika Kampuni ya JATU ambalo linatumika kuzalisha mafuta ya kula ya alizeti. Mafuta ya alizeti yanazidi kupata umaarufu mkubwa na hivyo uhitaji wake kuwa mkubwa kutokana na faida zake kiafya katika mwili wa mwanadamu.

Kampuni inaendesha kilimo cha alizeti katika wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na wanachama wake ili kujihakikishia malighafi ya kutosha kwa bidhaa ya alizeti.

Msimu wa alizeti huanza kuanzia mwezi Disemba hadi mwezi Juni ambapo wakulima wengi huwa katika mavuno. Hivyo mwanachama ambaye atahitaji kuwekeza katika kilimo cha Alizeti anatakiwa ajitahidi apate shamba mapema ili awahi kupata nafasi ya kuwekeza katika kilimo hiki.

Kwa msimu wa mwaka 2020-2021 tunategemea kulima ekari 5000 za alizeti katika wilaya ya kiteto. Muwekezaji anaweza kuwekeza kuanzia ekari 1 na kuendelea.

Gharama za uwekezaji na matarajio kwa ekari 1;

ZaoKukodi shambaKununua shambaGharama za kilimoMatarajio ya maguniaBei kwa kiroba(70kg/b)MauzoFaida
Alizeti50,000/=750,000/=613,800/=1652,500/=840,000/=226,200/=

2.Mahindi

This image has an empty alt attribute; its file name is artboard-4-1.png

Mahindi ni moja ya zao muhimu sana la chakula, na ni aina ya nafaka inayotumiwa zaidi kama chakula hapa nchini Tanzania. Mahindi huzalisha bidhaa ya unga wa dona na sembe ambao kampuni ya JATU huiuza kwa nembo yake. Kampuni inamiliki kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo kibaigwa mkoani Dodoma na sasa tunaendelea na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kisasa katika wilaya ya kiteto Mkoani Manyara. Tunalima mahindi kwa kushirikiana na wanachama wetu ili kuweza kupata malighafi za kutosha kuhudumia viwanda vyetu na wanachama wetu ambao hununua bidhaa za sembe na dona kupitia mfumo wa JATU. Mahindi hulimwa zaidi mkoa wa manyara wilaya ya kiteto, JATU tuna kituo cha kudumu katika eneo la matui Kijiji cha kazi ngumu, Kupitia kituo hiki Kampuni inao wataalamu wanaosimamia na kuratibu zoezi zima la kilimo cha mahindi kuanzia kutafuta mashamba, kuandaa, kupanda hadi kuvuna na kuhifadhi.

Msimu wa kulima mahindi katika eneo la kiteto huanza kuanzia mwezi November hadi mwezi June ambapo wakulima wengi huanza kuvuna mazao yao. Hata hivyo kutokana na uhitaji mkubwa wa maeneo ni vyema kuanza kutafuta mashamba mapema aidha kwa kununua au kwa kukodi.

Kwa msimu wa mwaka 2020-2021 tunategemea kulima angalau ekari 5000 za mahindi katika wilaya ya kiteto. Uwekezaji/Umiliki wa shamba unaanzia ekari 1 na kuendelea.

Gharama za uwekezaji na matarajio kwa ekari 1;

ZaoKukodi shambaKununua shambaGharama za kilimoMatarajio ya maguniaBei kwa kiroba(90kg/b)MauzoFaida
Mahindi50,000/=750,000/=668,800/=3083,700/=2,511,000/=1,842,200/=

3.Mpunga

This image has an empty alt attribute; its file name is artboard-3-2.png

Mpunga ni zao la pili la chakula kwa umuhimu linalolimwa na kusimamiwa na kampuni katika mkoa wa Morogoro. Umuhimu wa zao hili umeongezeka kutokana na jamii za mijini na vijijini kupendelea zaidi kutumia bidhaa hii na kulifanya zao hili kuwa la chakula na biashara. Zao hili utupatia bidhaa ya mchele. Kampuni inamiliki kituo cha kuzalisha na kufungasha mchele kilichopo wilaya ya kilombero mkoa wa Morogoro, katika kituo hiki kampuni pia inaendesha kilimo cha kisasa cha mpunga kwa kata za jirani zinazozunguka kituo cha JATU. Miongoni mwa kata ambazo JATU inaendesha kilimo ni pamoja na Mbingu, Igima, Mofu, Chita na Mlimba.

Kampuni hutafuta na kukodi au kununua mashamba kwa niaba ya wanachama na wanachama hulipia gharama zote za usimamizi na uendeshwaji wa mradi kuanzia kuandaa mashamba hadi kuvuna. Baada ya kuvuna mazao yote uhifadhiwa katika maghala maalumu ya kampuni yakisubiria mkulima afanye maamuzi ya kuuza au kukoboa mchele wake kupitia kituo cha kukoboa mchele cha JATU kilichopo Tandale, Mbingu.

Ratiba ya zao hili huanza kuanzia mwezi Octoba hadi mwezi Juni au Julai ambapo wakulima wengi huanza kuvuna mavuno yao. Hata hivyo kwa zoezi la kununua au kukodi shamba mchakato unatakiwa kuanza mapema ili kuweza kupata mashamba mazuri yasiyo twamisha maji muda mrefu na hivyo kuepusha hasara inayoweza kusababishwa na mafuriko

Kwa msimu wa mwaka 2020-2021 tunategemea kulima angalau ekari 5000 za mpunga katika wilaya ya kilombero. Uwekezaji/umiliki wa shamba unaanzia ekari 1 na kuendelea.

Gharama za uwekezaji na matarajio kwa ekari 1;

ZaoKukodi shambaKununua shambaGharama za kilimoMatarajio ya maguniaBei kwa kiroba(100kg/b)MauzoFaida
Mpunga100,000/=1,000,000/=904,200/=25112,000/=2,800,000/=1,895,800/=

4.Maharage

This image has an empty alt attribute; its file name is whatsapp-image-2020-03-20-at-4.56.57-pm-1-1.jpg

Maharage ni moja ya zao muhimu kwaajili ya lishe ya binadamu na hutumiwa kama mboga pendwa na jamii nyingi za kiafrika. Kwa nchi yetu ya Tanzania zao hili hutumiwa kwa wingi katika lishe ya kila siku katika familia. Maharage hulimwa na JATU kwa kushirikiana na wanachama wake katika mkoa wa Tanga kituo cha Kibirashi kilichopo wilaya ya Kilindi.

Katika kituo hiki JATU inalima, inaandaa na kufungasha maharage katika mifuko maalumu na kuyauza kwa wateja wake kupitia mfumo maalumu wa JATU. Mkulima wa JATU anaweza kukodi au kununua shamba katika eneo hili Kwa kutumia mfumo maalumu wa manunuzi wa kampuni (Jatu App) au kwa msaada wa wataalamu waliopo katika Kampuni ya JATU.

Msimu wa kilimo cha maharage katika mkoa wa Tanga, wilaya ya kilindi huanza mwezi February hadi July ambapo wakulima wengi huwa katika mavuno. Kutokana na uhitaji wa mashamba ni muhimu kuanza kutafuta mashamba mazuri mapema iwezekanavyo.

Kwa msimu wa mwaka 2020-2021 tunategemea kulima angalau ekari 3000 za maharage katika wilaya ya kilindi. Mkulima anauwezo wa kuwekeza kuanzia ekari 1 na kuendelea.

Gharama za uwekezaji na matarajio kwa ekari 1;

ZaoKukodi shambaKununua shambaGharama za kilimoMatarajio ya maguniaBei kwa kiroba(100kg/b)MauzoFaida
Maharage100,000/=850,000/=844,800/=15195,000/=2,925,000/=2,080,200/=

5.Kilimo cha Matunda

This image has an empty alt attribute; its file name is cropped-uabq5lgpjqd3ddo6ve2dfw.jpg

Matunda ni mazao ya muda mrefu ambayo yameanzishwa na kampuni ili kuwezesha kampuni kuanza kuzalisha bidhaa zitokanazo na matunda hasa machungwa, maembe, parachichi na nanasi. Bidhaa ambazo Kampuni inategemea kuzalisha ni pamoja na juisi na matunda freshi.

Kilimo cha matunda na JATU tayari maandalizi yameanza na kinafanyika katika mkoa wa tanga wilaya ya muheza na handeni. Katika awamu ya kwanza ya kilimo hiki ambayo inategemewa kuanza mwaka huu wa 2020 tutaanza na kilimo cha zao la machungwa, na baada ya kukamilisha upandaji wa zao hili tutaanza tena awamu ya pili ambayo itakuwa na mazao mengine ya matunda kwa kadri itavyotangazwa na Kampuni.

Zao la matunda kwa kuwa ni la muda mrefu, mashamba yatakayotumika ni yale ya kudumu tu, yaani mkulima anashauriwa kununua na kumiliki shamba lake kwani hatutakuwa na mashamba ya kukodi.

Kwa msimu wa mwaka 2020-2022 tunategemea kulima angalau ekari 1000 za machungwa katika wilaya ya Muheza na Handeni.

Gharama za uwekezaji na matarajio kwa ekari 1 msimu wa kwanza;

ZaoKununuaGharama za kilimoMatarajio ya mavuno
(Machungwa)
Bei kwa chungwaMauzo

Faida
Machungwa1,000,000/=Year One: 2,400,000/=
Year Two: 1,500,000/=
Year Three: 1,800,000/=
Total: 6,000,000/=
50000100/=Kwa misimu 2@5,000,000
= 10,000,000/=
-Mwaka wa kwanza wa mavuno =4,000,000/=
-Mwaka wa pili na kuendelea =8,000,000/=

Kwa maelezo zaidi juu ya namna ya kujiunga na kilimo cha JATU wasiliana nasi: +255 758 396 767

Kwa maelezo zaidi juu ya kilimo cha machungwa pakua nakala hii:namna-ya-kumiliki-na-kuhudumia-shamba-la-machungwaDOWNLOAD

Kwa maelezo zaidi juu ya ratiba ya kilimo na JATU pakua nakala hii:Ratiba ya Msimu wa Kilimo 2020 (3)DOWNLOAD

MASOKO (JATU MARKET)

 • Masoko ya uuzaji wa bidhaa za kampuni ya JATU ni ya mfumo wa kimtandao (Network Marketing). Biashara ya masoko ya mtandao ni ya kupashana habari kati ya mtu mmoja hadi mwingine kuhusu huduma na bidhaa za kampuni ambazo hupatikana kupitia mfumo wetu (Jatu Market).
 • Jatu Sokoni (Jatu Market) ni mfumo unaotumiwa na kampuni ya Jatu katika uuzaji wa bidhaa zake na za mabalozi wake.
 • Ingia playstore pakua mfumo wa Jatu Sokoni kwenye simu yako, jisajili na uanze kufanya manunuzi ya bidhaa zetu.
 • Balozi ni mwakilishi wa kampuni katika kuuza au kusambaza bidhaa za kampuni, pia balozi wa JATU anaweza kuwa mwanachama mbunifu ambae anaweza kubuni bidhaa yake na kutumia masoko ya JATU kujitengenezea kipato.
 • Mwanachama anaweza kutengeneza mtandao wake kuanzia kizazi cha kwanza hadi kizazi cha tano na vizazi vyake vinapofanya manunuzi kupitia mfumo wa Jatu Sokoni mwanachama hupatiwa gawio kila mwezi ambayo ni jumla ya 40% ya faida yote iliyoingia.
 • Mwanachama/Mteja anaponunua bidhaa yoyote kupitia mfumo wa Jatu Sokoni anapata gawio la faida la kila bidhaa atakayonunua.
 • Gawio la faida hutolewa kila mwisho wa mwezi kupitia namba ya simu mwanachama aliyojisajilia.
 • Mwanachama/Mteja anapowapasha habari ndugu, jamaa na rafiki zake anatengeneza mtandao wake ambao kupitia huo mtandao anauwezo wa kupata gawio kubwa zaidi. Kila mtu aliyepo kwenye mtandao wake anapofanya manunuzi kupitia mfumo na kulipia, mwanachama anapata gawio lake pamoja na la wana mtandao wake.
 • Mteja anapofanya manunuzi hupelekewa bidhaa zake mahali popote atakapohitaji apelekewe.

MCHANGANUO WA FAIDA

Mtandao wa Masoko wa JATU PLC ni chanzo cha kipato kwa wote walioshiriki kuanzisha JATU, kulea wazo na wanaoshiriki kuleta wateja wa kununua bidhaa za JATU PLC kupitia JATU App.

Kanuni ya JATU inagawa FAIDA kwa kuzingatia mfumo huu kwa sehemu mbili;

1. JATU PLC

2. MTANDAO

JATU PLC ndio kampuni inayobeba na kusimamia mfumo mzima, kwa sababu hii kampuni inapata gawio la faida ya asilimia arobaini (40%) kwa kila bidhaa inayouzwa kupitia mfumo wa JATU.

MTANDAO, huu unaanzia waasisi wa mfumo, walezi(mabalozi) wanaolea wanachama huko mtaani na huishia kwa wateja wanaonunua bidhaa kwa matumizi yao binafsi. Kwa ujumla wao wote wanapewa gawio la asilimia sitini (60%) kutokana na faida inayopatikana kwa kila bidhaa inayouzwa JATU.

MTANDAO huu umegawanyika kwa sehemu kuu nane(8) kama ifuatavyo;

1. WAZAZI(FOUNDERS), Hawa ni waanzilishi wa wazo la JATU PLC, wao kwa umoja wao wanalipwa asilimia 10% ya faida yote inayopatikana kwa kila bidhaa kila mwezi.

2. BALOZI, hawa ndo wasimamizi wakuu wa mfumo huu huko mtaani, wanakutana na wanachama na kuwalea (kwa kuwapa elimu na ushauri) ili kuhakikisha wanajenga mtandao imara, kwa majukumu na umuhimu wao wanapata gawio la faida asilimia kumi (10%) kwa kila bidhaa iliyouzwa kwa kutumia namba yao ya kibalozi. (Kumbuka unaponunua chochote kwa app ya JATU lazima uchague balozi wako).

3. SPONSOR (WW mdhamini) huyu kazi yake kubwa ni kujenga mtandao, sponsor ndo mteja wa kwanza katika huu mfumo, yeye anapata asilimia kumi ya gawio kwa kila bidhaa anayonunua kwa JATU kupitia akaunti yake.

Lakini pia anapata asilimia zingine thelathini (30%) kutokana na mtandao wake wa vizazi atapotengeneza kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha tano kama ifuatavyo;

 • Kizazi cha kwanza(K1) – 10%
 • Kizazi cha pili (K2) – 8%
 • Kizazi cha tatu (K3) – 6%
 • Kizazi cha nne (K4) – 4%
 • Kizazi cha tano (K5) – 2%

______________________________________________________________________

Ukijumlisha hatua zote hapo juu utapata jumla ya asilimia sitini (60%) kama ifuatavyo;

1. Wazazi – 10%

2. Balozi – 10%

3. Sponsor – 10%

4. K1 – 10%

5. K2 – 8%

6. K3 – 6%

7. K4 – 4%

8. K5 – 2%

_____________

JUMLA – 60%

MIKOPO (JATU SACCOS LTD)

This image has an empty alt attribute; its file name is dsc_0033.jpg

Kampuni ya JATU ushirikiana na Jatu Saccos Limited kuwafadhili wakulima wake.

Jatu Saccos Limited ni chama cha ushirika kilichoanzishwa na kampuni ya Jatu Plc kwa lengo la kuwezesha wanachama wake wanaoshiriki katika miradi ya kilimo  kupata mikopo ya kuwawezesha kumudu fursa hii na mkopo huu hauna riba kabisa. Lakini chama hiki hakijaishia hapo kwani kinatoa mikopo kwa wanachama wabunifu na wafanyabiashara ili kumudu gharama katika ubunifu wao na kukuza mitaji pia.

Mikopo ya kilimo

 • Mkopo huu wa kilimo hutolewa mara tatu ya akiba aliyoweka mwanachama,
 • Mwanachama huchangia 1/3 ya gharama ya kilimo husika na 2/3 ukopeshwa na Jatu Saccos kwaajili ya kukamilisha gharama za kilimo.
 • Mwanachama huruhusiwa kuchangia kidogo kidogo akiba yake ili kukamilisha 1/3 ya gharama za kilimo.
 • Mkopo huu hauna riba.
 • Mkopo huu utarejeshwa baada ya msimu wa kilimo kuisha na mkulima kuuza mazao yake.
 • Mkopo huu utadhaminiwa na mwanachama mwenyewe pamoja na akiba yake.

Mchanganuo wa uwekaji wa akiba na mkopo wa kilimo kwa msimu wa kilimo 2020 – 2021 kwa kila zao;

ZaoMakadirio ya GharamaAkiba (1/3 Tshs)Mkopo (2/3 Tshs)
Mpunga904,200/=301,400/=602,800/=
Mahindi668,800/=222,934/=445,866/=
Alizeti613,800/=204,600/=409,200/=
Maharage844,800/=281,600/=563,200/=

Baada ya mkulima kukamilisha akiba ya kilimo husika anapaswa kufanya yafuatayo;

 1. Alipie shilingi elfu kumi (10,000/=) kwaajili ya kujaza fomu ya maombi ya mkopo wa kilimo husika.
 2. Alipie gharama za uendeshaji wa mkopo /loan processing fee 3%

Mchanganuo wa 3%

Loan processing fee 3% /gharama za uendeshaji wa mkopo, hii ni ada anayopaswa mkulima yoyote wa zao fulani alipie mara baada tu ya kukamilisha kulipia gharama zote za kilimo anachotarajia kulima.

Ada hii 3% inahusisha vitu viwili ambavyo ni

 • 1% ada ya mkopo
 • 2% bima ya mkopo

3% inachajiwa kwenye kila mkopo mkulima atakao kopeshwa kwa kila ekari.

Mfano 1; Mkulima anaelima kwa mkopo shamba heka moja basi atalipia 3% ya mkopo aliokopeshwa kwenye hio ekari moja.

Mfano 2; Mkulima anaelima kwa mkopo shamba ekari tatu basi atailipia 3% ya mkopo atakaokopeshwa kwa kila ekari yaani atalipia kutokana na idadi ya hekari anazolima.

NB; Hii inategemeana na mkopo anaopewa mkulima kwa kila ekari, kuna wanaopata mkopo 2/3 kuna wanaopata mkopo nusu gharama na kuna wanaopata mkopo robo yani 1/3 hii inategemea na huyo mteja kaanza kuweka lini akiba yake ya kulimiwa shamba.

JATU – Jenga Afya Tokomeza Umasikini

2 thoughts on “HAKIKI ORODHA YA WAKULIMA WA JATU MSIMU 2020/2021 KWA AMBAO BADO HAMJAKODI, ENDELEA KUKODI AU KUNUNUA MASHAMBA KUPITIA JATU MARKET APP ILI USIKOSE NAFASI MSIMU HUU

 1. Orodha ya washiriki wa kilimo 2020/2021 haifunguki sasa ili tuone maana wengine tuliambiwa tupeleke mahitaji yetu na tukafanya hivyo baada ya kushindwa kutoa order kwa mtandao sijui mmetufikiriaje npaka sasa. Kwa mfano mimi nilitaka eka 10 mpunga, 5 maharage na 5 mahindi. Mpaka sasa sielewi na ni mwanachama nimeshiri kilimo msimu uliopita.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s