JATU PLC YAJIPANGA KUONGEZA THAMANI YA ZAO LA MACHUNGWA HANDENI-TANGA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

JATU PLC kampuni inayoendesha miradi mikubwa ya kilimo nchini ikiwemo na mradi wa kilimo cha matunda aina ya machungwa wilayani Handeni, Tanga imejipanga kuongeza thamani kwenye zao hilo ili kuongeza tija kwa wakulima. Mkurugenzi wa JATU PLC Ndg. Peter Isare aliongea hayo kwenye ziara ya watumishi wa wizara ya kilimo wakiongozwa na Ndg. Revelian Ngaiza (Mratibu wa Mkakati wa Vijana Kilimo) walipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi ya kilimo inayosimamiwa na kuendeshwa na kampuni ya JATU. “Kilimo cha machungwa ni mradi ambao mwaka 2019 mwishoni tuliuanza kwa kufanya utafiti wa kina ili kupata mashamba yenye tija kwenye wilaya za Handeni na Muheza lakini tukafanikiwa kupata shamba zuri katika kijiji cha Nkale hapa Handeni ambapo tutaanza na ekari 500.

JATU imeamua kulima machungwa eneo hili kutokana na jiografia ya eneo hili ni zuri sana na pia kuna wakulima wengi wa matunda katika eneo hili. Tumelenga kuwa na uzalishaji mkubwa wa vinywaji aina ya juisi ambavyo yatatokana na matunda tutayozalisha kutoka eneo hili. Shamba hili litatuwezesha kuwafikia na wakulima wengine ambao ni jirani na eneo hili hivyo watapata soko la uhakika.

Tumeamua kuwekeza eneo hili kutokana na ripoti maalumu ilioandaliwa na Wizara ya kilimo mwaka 2017 ikiainisha kila wilaya na mazao yanayokubali hivyo wilaya hii ya Handeni imeainishwa kufanya vizuri kwenye hili zao la machungwa.”

JATU inaendelewa kuwakumbusha wanachama na wadau wote ambao wangependa kushiriki kwenye miradi ya kilimo msimu mpya wa 2020/21 kuchangamkia hii fursa kabla ya muda kuisha.

JATU – Jenga Afya Tokomeza Umasikini

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s