Habari njema kwa wakulima wetu waliowekeza katika kilimo cha mpunga. Muda wa mavuno sasa umewadia, mpunga wetu umeshakomaa tayari kabisa kwa kuvunwa leo tarehe 21.05.2020 tunaanza rasmi zoezi la uvunaji. Kwa wakulima ambao wamelima zao hili na watapata nafasi ya kufika shambani Morogoro Mbingu kushuhudia zoezi hili wanakaribishwa sana na kwa wale ambao watashindwa kufika tutaendelea kuwapa mrejesho wa kila hatua tutakayofikia. Kwa wakulima ambao wanatamani kuwekeza katika kilimo hiki cha mpunga msimu ujao 2020-2021 nafasi bado zipo za kutosha wahi kukodi au kununua shamba lako sasa ili nawe uwe mmoja kati ya watakaonufaika na kilimo hiki chenye tija. Tukabidhi shamba lako tupo tayari kukuhudumia.
Ni habari njema hii kwa kweli,
LikeLike
Habari Mkuu,
Karibu sana ujiunge nasi tuendelezee huu mchakato wa kuboresha kilimo na wakulima kiujumla
LikeLike
Hello ningependa kufahamu gharama zakulimiwa kwa hekari moja ni shillings ngapi ili niweze kujua naitaji kiasi gani niweze kuwekeza kwa msimu ujao
LikeLike
Habari Irene,
Kufahamu juu ya gharama mbalimbali za kilimo na JATU wasiliana nasi 0658126324
LikeLike
I would like to joing in this campany because I have been motivated and I will follow all rules and regulations of the campany
LikeLike
Hello Ally,
Your welcome to join with us kindly visit our offices at Posta Samora street for further details contact us +255658126324
LikeLike
Jaman kilimo cha Alzet 2019-2020 kimefikia wap sasahv
LikeLike
Habari Martin,
Tunategemea kuanza kuvuna zao la alizeti kuanzia mwishoni mwa mwezi huu, kwasasa tunasubiri yakauke vizuri kabla ya kuanza kutumia mashine kuvuna
LikeLike