FAHAMU KUHUSU JATU PLC – KUJIUNGA UANACHAMA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

KUJIUNGA JATU PLC

Kwa wote walioelewa kuhusu JATU na wako tayari kujiunga tafadhali waingie playstore/appstore wapakue App yetu na waweze kujiunga Kupitia App ya Jatu au kama yupo karibu na ofisi zetu basi wafike ofisini moja kwa moja ili kuweza kujifunza zaidi (Posta PSSSF House Ghorofa Na. 06) au karibu na branch zetu zilipo mikoani kama vile Arusha, Morogoro, Dodoma, Kiteto Manyara, Mtwara, Mwanza. Pia unaweza kutuma mfumo huu kuminya sehemu iliyoandikwa jiunge hapa ukaweza kujiunga au kupakua Apps ya JATU katika playstore kwa kuandika neno JATU kisha ukaunda akaunti mpya moja kwa moja na kuweza kupata namba ya uanchama.

Kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutupigia: 0800 7500 97

gharama za kujiunga

Kwa yeyote atakayetaka kujiunga na JATU Plc atatakiwa kujaza fomu maalumu ya uanachama ambayo inapatikana kwenye tovuti yetu na kwenye Application yetu iliyopo playstore unachotakiwa ni kusoma maelezo na kujaza taarifa zako ambapo zitatufikia moja kwa moja kama utajaza fomu yetu kwa usahihi na kupewa namba ya utambulisho ya Uanachama wa JATU. Gharama yake fomu hiyo ni shilingi elfu Thelathini tu (30,000/=) na atakuwa ni mwanachama wa kawaida mwenye haki ya kununua na kushiriki na kupata huduma zinazotolewa na JATU Plc, lakini unaweza shiriki fursa hii kwa mkopo kwa kujaza fomu hiyo bure kabisa lakini baada ya kuanza kufanya manunuzi deni lako litaanza kukatwa kidogo kidogo mpka kukamilika kiingilio cha Tsh. 30,000/=.

Gharama ya hisa moja ni shilingi elfu mbili na mia tano tu (2,500/=). lakini hii ni Mpaka Jatu watakapokuwa tayari washaorodheshwa soko la Hisa la Dar es salaam, kwa Hisa za Ndani zimesitishwa Kuuzwa.

Kwa mwanachama atakayehitaji kujiunga kwenye mradi wa kilimo atatakiwa kuwasiliana na namba +255 657 779 244 ili kupewa ufafanuzi zaidi kuhusiana na kilimo na JATU Pia unaweza tembelea https://jatukilimo.com/ kwa habari zinazohusu kilimo.

AKAUNTI ZA MALIPO JATU PLC

NJIA YA BENKI (NMB): Unaweza kufanya malipo yako kwa kutumia benki ya NMB kwa akaunti namba zifuatazo kutokana na huduma.

MALIPO YA UNUNUZI WA MASHAMBA NA MAMBO YA KILIMO: Benki: NMB  Akaunti Namba: 20710026988 Jina: JATU KILIMO

MALIPO YA BIDHAA ZA JATU: Benki: NMB  Akaunti Namba: 23610002972 Jina: JATU MAUZO

MALIPO MENGINE YANAYOHUSU JATU: Benki: NMB  Akaunti Namba: 20710025732 Jina: JATU PLC

MALIPO YA KUWEKA AKIBA NA MALIPO MENGINE YA SACCOS: Benki: NMB  Akaunti Namba: 23610003111 Jina: JATU SACCOS LTD

MALIPO KWA MITANDAO YA SIMU

Kwa watumiaji wa Vodacom unaweza fanya malipo kupitia M-PESA:

1. Ingia M-Pesa  * 150*00#

2. Chagua 4 (Lipa kwa M Pesa)

3. Chagua 4 (Weka namba ya Kampuni)

4. Ingiza namba ya kampuni ambayo ni 370033

5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (sababu ya Malipo ni nini?)

6. Weka kiasi

7. Weka namba ya siri

8. Bonyeza 1 kuthibitisha

9. Ombi lako litatumwa kwenda JATU MAUZO

10. Kisha tuma taarifa zako, Jina Lako Kamili, na Malipo uliofanya

Kwa watumiaji wa Tigo unaweza fanya malipo kupitia Tigo-PESA:

1. Ingia Tigo Pesa  * 150*01#

2. Chagua 4 (Lipa kwa Tigo Pesa)

3. Chagua 4 (Weka namba ya Kampuni)

4. Ingiza namba ya kampuni ambayo ni 370033

5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (sababu ya Malipo ni nini?)

6. Weka kiasi

7. Weka namba ya siri

8. Bonyeza 1 kuthibitisha

9. Ombi lako litatumwa kwenda JATU MAUZO

10. Kisha tuma taarifa zako, Jina Lako Kamili, na Malipo uliofanya

aina za uanachama

JATU ni Kampuni ya umma ambayo ina aina zifuatazo za wanachama;

MWANACHAMA MTEJA:

Huyu ni mwanachama ambaye anajiunga na kampuni baada ya kupashwa habari na mwenzake/kizazi/mtu wa juu yake kuhusu JATU na kuamua kujiunga kwa lengo la kununua bidhaa za JATU. Hawa wanachama wanatambulika kwa namba zao za uanachama ambazo zinapatikana mara baada ya kujaza fomu ya usajili kupitia mfumo wa JATU (JATU APP). Wanachama hawa wanapata faida ya gawio la faida kutoka kwa kampuni kila mwezi Kutokana na matumizi yao na wana mtandao wao.

MWANACHAMA BALOZI:

Hawa ni wanachama ambao baada ya usajili, wanajikita zaidi katika kuuza bidhaa za JATU au kubuni bidhaa zao na kuziuza katika mfumo wa JATU. Wanajengewa uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanachama wapya na kuwa mabalozi wao wakati wa usajili. Wanalipwa na Kampuni Kulingana na idadi ya watu au wateja waliowahudumia na faida waliyoingiza.

WANAHISA:

Hawa ni wanachama ambao wanamiliki sehemu ya kampuni kulingana na hisa zao, ni wamiliki wa kampuni na wanastahili gawio la kila mwaka ikiwa kampuni imepata faida katika mwaka wa fedha.

WAKULIMA:

Ni wanachama wenye hisa kadhaa kwenye kampuni lakini pia wanafanya kilimo chini ya usimamizi wa Kampuni. Wanalima kwa pamoja na kuuza mazao yao kwa kampuni. Kampuni inawasaidia kufanya utafiti katika miradi yao, vifaa, zana, huduma za ugani, maghala na soko la uhakika kwa mazao yao.

4 thoughts on “FAHAMU KUHUSU JATU PLC – KUJIUNGA UANACHAMA, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s