FAHAMU KUHUSU JATU PLC- UTANGULIZI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

JATU– Kirefu cha jina JATU ni “Jenga Afya Tokomeza Umasikini”

JATU PLC ni Kampuni ya Umma yenye ukomo/umiliki kupitia hisa. Kampuni ilisajiliwa tarehe 20 Oktoba 2016 chini ya sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 na kupewa cheti cha usajili namba 130452 kilichotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Tanzania.

JATU PLC ni kampuni ya umma inayowaunganisha wakulima na kuwawezesha kulima pamoja kitaalamu kwa kutumia zana za kisasa na wataalamu waliobobea katika kilimo. JATU inawasaidia wanachama wake katika kutafuta mashamba mazuri, kubuni ni zao gani lilimwe kwa wakati gani, kampuni inahakikisha mashamba yamelimwa na kuandaliwa kitaalamu kabla ya kupanda zao husika, katika kupanda kampuni inahakikisha mbegu sahihi zimetumika, huduma ya mmea kwa kila hatua ndo jukumu kuu la kampuni ya JATU. Ni wajibu wa JATU kuhakikisha mteja anapata soko la uhakika kwa mazao yote ambayo amelima. Kampuni hununua mazao yote na baadaye kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa wanachama wake kwa mfumo wa biashara ya mtandao.

DIRA YA KAMPUNI

Kuwa kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora na kuwezesha upatikanaji wa kipato kwa kila mtu.

DHIMA YA KAMPUNI

Kutumia Rasilimali watu kwenye Kilimo, Viwanda na Masoko ya Mauzo ya bidhaa za chakula kwa wateja kupitia mfumo wa masoko ya mtandao na kuwawezesha kujenga afya na kutokomeza umaskini.

MALENGO MAKUU

Malengo makuu ya Kampuni yamegawanyika katika sehemu tatu (3) ;

(a) Kuunganisha wakulima, wakulima wadogo na watu wenye nia ya kufanya kilimo na kuwasadia kufanya kilimo cha kisasa na kwa pamoja.

(b) Kuanzisha viwanda Karibu na maeneo ya kilimo au mashamba na kuendesha shughuli za viwanda vya kuchakata mazao ya chakula.

(c) Kuendesha masoko ya mtandao katika kuuza bidhaa na huduma mbalimbali ili kuhakikisha ugawanaji wa faida baina ya wanachama.

MISINGI MIKUU YA JATU

Katika kampuni ya JATU kuna misingi mikuu mitano ambayo ni muhimu kwa kila mwanachama wa JATU kuijua na kuifanyia kazi mda wote awapo ndani na nje ya JATU.

 1. Umoja
 2. Bidii
 3. Ubunifu
 4. Uthubutu
 5. Huduma bora

HUDUMA ZA JATU

Kampuni ya Jatu inajihusisha na huduma kuu zifuatazo:

 1. UTAFITI: Tunafanya utafiti wa mazao na maeneo ya kulima/mashamba.
 2. KILIMO: Tunatoa zana za kilimo na pembejeo kwa wakulima/wateja wetu.
 3. MASOKO: Tunatoa masoko kwaajili ya mazao ya wateja wetu
 4. USAJIRI: Tunatoa mafunzo na kusajili watumiaji na wateja wa bidhaa zetu.
 5. SOKO LA MTANDAONI: Tunauza bidhaa zetu za chakula kupitia mfumo wa soko la mtandaoni la JATU.
 6. UJASIRIAMALI: Tunatoa/tunawezesha masoko kwa wajisiriamali wengine kupitia soko letu la mtandaoni.
 7. HUDUMA ZA SHAMBA: Tunatoa huduma za kuhudumia shamba kwa wakulima wetu.
 8. KUHIFADHI MAZAO: Tunatoa huduma yakuhifadhi mazao ya wakulima/wateja wetu baada ya mavuno.
 9. KUCHAKATA MAZAO: Tunachakata mazao na kufungasha bidhaa
 10. MASOKO YA MTANDAO: Tunatoa gawio kwa wateja wetu wote kulingana na manunuzi ya bidhaa zetu wanazofanya kwa mwezi kupitia mkakati wa soko la mtandao.
 11. USAMBAZAJI WA BIDHAA: Tunasambaza na kuwafikishia wateja wetu bidhaa ambazo wamenunua mpaka mlangoni.
 12. MIKOPO: Tunatoa mikopo rahisi na isiyokuwa na riba kwa wakulima wetu.
 13. VIWANDA: Tunawekeza kwenye viwanda vya kuchakata mazao pamoja na mashine za kutumika mashambani.

Mpango mkakati wa Kampuni ni kufikia wilaya zote za Tanzania kupitia Kilimo, Viwanda na Masoko ya mtandao. Kwa sasa, Kampuni inaendesha shughuli za Kilimo cha maharage wilayani Kilindi mkoa wa Tanga, Kilimo cha Mpunga wilayani Kilombero, Morogoro, Kilimo cha Mahindi na Alizeti huko Wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara na Kilimo cha matunda, Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

UHALALI WA KAMPUNI

Kampuni imesajiliwa nchini Tanzania na kupatiwa vyeti vya usajili na leseni kutoka mamlaka za serikali kama ifuatavyo;

Mnyororo wa thamani wa JATU PLC

WAANZILISHI WA JATU PLC

JATU ilianzishwa na vijana wakitanzania wakiongozwa na Peter Isare pamoja na wenzake; Mohamed Issa Simbano, Esther Philemon Kiuya, Charles Mwita Gichogo, Ekaudi Semkiwa, Paul Kapalata Msabila, Magreth Laurent Fabian, Kenneth Maganga, Claudia Albogast Simon, Moses William Lukoo, Esther Christian Marino & Mary Chulle.

OFISI ZETU

Kampuni ina aina tatu za ofisi kama ifuatavyo;

(a) Makao Makuu:

Makao makuu ya Kampuni yapo Dar es salaam, Wilaya ya Ilala Jengo la PSSSF ghorofa ya kumi na moja (11) kwenye makutano ya Mtaa wa Samora na Barabara ya Morogoro. Ofisi hii inafanya shughuli zote za kiutawala.

(b) Ofisi za Shamba:

Ofisi hizi zinapatikana kwenye maeneo ya uzalishaji ambayo yanajumuisha mashamba yanayomilikiwa na wanachama wa JATU na kusimamiwa na Kampuni na pia kwenye maeneo ambayo yana viwanda vya Kampuni. Ofisi hizo zinajumuisha Ofisi ya Matui iliyopo Wilaya ya Kiteto ambapo Kampuni inaendesha kilimo cha Mahindi na Alizeti; Ofisi ya Kilindi iliyopo eneo la Kibirashi kwa ajili ya kilimo na uchakataji wa maharage; Ofisi ya Kibaigwa iliyopo Dodoma ambapo kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na alizeti na Ofisi ya Kilombero iliyopo Mbingu ambapo tunaendesha kilimo cha Mpunga kiwanda cha kukoboa mpunga.

(c) Ofisi za Masoko:

Ofisi hizi zinapatikana kwenye maeneo yenye watu wengi kama vile kwenye Wilaya na makao makuu ya mikoa. Ofisi hizi zinajumuisha Ofisi za Mtwara mjini(jengo la PSSSF gorofa ya Tatu, wengi wanapaita NMB ya mjini karibu na stend kuu ya zamani ya mtwara mjini), Mwanza(Nyamagana katika Mtaa wa Nyerere jengo la CCM Ghorofa ya Pili), Dodoma(Jengo la Dodoma Media College lililopo round about ya bahi road njia ya singida), Arusha(Kaloleni katika jengo la Kondo Investment ghorofa ya pili room namba 221. Jengo hili linatazamana na kanisa LA Pentekoste la kaloleni) na Posta Dar es salaam(Jengo la PSSSF ghorofa ya sita mtaa wa Samora) . Ofisi hizi zimejikita katika masoko na kuuza bidhaa na huduma za JATU.

MAWASILIANO

EMAIL: info@jatu.co.tz

Website: http://www.jatu.co.tz and http://www.jatukilimo.com

Instagram: @jatu_plc @jatu_pesa @jatu_talk

Facebook: @jatu_plc @jatu_pesa @jatu_talk

Twitter: @jatu _plc @jatu_pesa @jatu_talk

Youtube: @Jatu TV

Call Free: 0800 7500 97

Whatsapp: +255657779244

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s