Habari,
Tungependa kuwajulisha wanachama wa JATU na wadau wetu wote wa kilimo kuwa tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa baraka tele anazozidi kuziachilia katika ardhi ya Kilindi Tanga. Kilimo cha Maharage kinaendelea vizuri sana na kinaleta matumaini makubwa kwa wawekezaji wa zao hili. Kwasasa bado tunaendelea na zoezi la upandaji wa maharage na habari njema ni kwamba katika maeneo ambayo tulishaanza kuyapanda siku saba zilizopita tayari maharage yameshaanza kutoka kwa kasi ya ajabu.
Usikose kushiriki katika kilimo hiki chenye tija msimu unaofata 2020 – 2021. Tukabidhi shamba, Wewe endelea na shughuli zako, Tukutane sokoni. “Lima Bila Stress na JATU”.