FAHAMU KINACHOENDELEA SASA KILIMO CHA ALIZETI NA JATU KITETO, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Karibu ujiunge nasi JATU PLC wataalamu wa kilimo kisicho na stress tunajivunia alizeti yetu inavyozidi kunawili kipindi hiki cha mvua shambani Kiteto, Manyara. Hali ya mazao ni nzuri sana na inaleta matumaini makubwa kwa wanachama juu ya kupata mavuno ya kutosha msimu huu. Timu yetu ya wataalamu wa kilimo inaendelea kufuatilia mwenendo wa ukuaji wa mazao ili kuhakikisha hayasumbuliwi na wadudu wala magonjwa.

JATU PLC ni kampuni ya umma ambayo imejikita kwenye uwekezaji wa kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji katika maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wanachama wake. Moja ya miradi ya kilimo inayoendeshwa na JATU ni pamoja na kilimo cha alizeti kinachofanyika Kiteto, Manyara, ambacho kina takribani ekari 5000. Nje ya alizeti JATU inaendesha miradi ya kilimo cha mahindi, mpunga, maharage na machungwa.

Alizeti ni moja ya mazao muhimu kwenye chakula kwani hutupatia mafuta ya kula yasio na lehemu(choresterol) ambayo yamependekezwa na wataalamu wa afya kwa matumizi ya kila siku. JATU hulima alizeti na kuzalisha mafuta ya kula ya JATU Alizeti ambayo yana ubora na ladha ya kipekee pia ni chaguo namba moja sokoni. Lengo la JATU ni kuhakikisha watanzania wanaweza kujenga afya na kutokomeza umasikini kupitia fursa za kilimo, viwanda, mikopo na masoko ya bidhaa za chakula. Kilimo cha JATU kimeboreshwa kwa kuwawezesha wanachama kushiriki kilimo pasipo usumbufu wowote na JATU ikisimamia mashamba yao. Pia JATU huwapatia mikopo isio na riba wakulima wake kisha hurejesha hizo fedha baada ya kuuza mazao waliovuna.

WEKEZA NA JATU KWA KILIMO CHENYE TIJA KISICHO NA STRESS

3 thoughts on “FAHAMU KINACHOENDELEA SASA KILIMO CHA ALIZETI NA JATU KITETO, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

  1. Mpo vzr. Naomba link ya wasap nijifunze zaidi namna ya kujiunga na kujua juu ya kilimo Cha alizeti na mazao mengine pia.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s