FAHAMU KUHUSU KILIMO CHA MAHARAGE NA JATU KILINDI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Habari,

Tunapenda kuwajulisha wakulima wanaoshiriki kilimo cha maharage na JATU Kilindi, Tanga kuwa maandalizi ya awali ya kuandaa mashamba tayari yamekamilika na sasa baada ya zoezi la kulima kwa awamu ya pili na kuchabanga udongo kisha kulinganishwa kwa kutumia rotaveta, tumeanza rasmi zoezi la kupanda mbegu kwa kutumia mashine za kupandia(planters).

Zoezi la upandaji limechelewa kidogo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo kupelekea kusogezwa mbele kidogo muda wa kupanda. Hata hivyo kwasasa hali imeimalika na zoezi la upandaji limeanza tangu 10/04/2020. Zao la maharage ni kati ya mazao ambayo hutumia muda mchache sana shambani ambapo hutumia miezi mitatu hadi minne hadi kuvuna hivyo bado tupo ndani ya matarajio yetu tuliojiwekea. Wataalamu wetu wa kilimo wanasimamia zoezi hili na kuhakikisha kila hatua inakamilika kwa wakati na kuleta matokeo chanya kwenye kilimo chetu.

Pia tungependa kuwakaribisha wadau wengine wa kilimo kujiunga nasi tushirikiane kuboresha kilimo cha maharage na kuhakikisha zao hili muhimu kwa chakula cha kila siku linaleta tija kwa wakulima.

7 thoughts on “FAHAMU KUHUSU KILIMO CHA MAHARAGE NA JATU KILINDI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

 1. mimi ninataka kulima maharage lakini ni mwakani ili niweze kuandaa fedha na kutumia saccos niweze kulima heka 10.Je nikiasi gani ninaweza kupump inn kwa project hii?

  Like

  1. Habari Prosper,

   Kushiriki kilimo cha maharage inabidi kwanza ukodi shamba kwa ekari 1 ni shillingi 100,000/= pili kuweka akiba ya kuhudumia shamba kwa ekari 1 ni 295,000/=. Karibu sana kwa mawasiliano zaidi 0658126324

   Like

 2. Tunawashukuru sana Kampuni ya JATU hasa kwa Mikakati Mizuri na yenye Kuleta Tija katika Secta ya Kilimo Tanzania, Mimi Tayari Nishaweka Order na kulipia Ekari 5 kwa ajili ya kilimo cha Maharage kwa Msimu Ujao, Je Natakiwa kuweka SACCOS Kwa Muda gani ili niweze kupata Mkopo kwa ajili ya Kilimo?? Na fedha hiyo Inaweza kuwekwa kwa Mkupuo yote??

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s