TANGAZO LA KAZI YA MKAGUZI WA NDANI JATU SACCOS

TANGAZO LA KAZI

Chama cha akiba na mikopo cha Jatu kinachojumuisha wanachama wa Kampuni ya Jatu PLC  kinatangaza nafasi za kazi ya mkataba ya mkaguzi wa ndani kwa watanzania wenye sifa kama zilizoainishwa hapo chini:

 NAFASI YA MKAGUZI WA NDANI (1).

Atakuwa anatekeleza majukumu ya ukaguzi na uthibiti wa ndani katika kuhakikisha kuwa sheria, kanuni,masharti,sera, maazimio ya Vikao na mikitano pamoja na nyaraka za mrajisi vinazingatiwa katika uendeshaji wa JATU SACCOS na kuwa SACCOS inaendeshwa na kuongozwa katika hali iliyo bora.

Atakuwa anawajibika kwa meneja na atakuwa mshauri wake katika masuala ya mifumo thabiti ya uthibiti wa ndani na taarifa yake itapelekwa kwa meneja, bodi ya uongozi na kamati ya usimamizi.

SIFA ZA MKAGUZI WA NDANI

  1. Anaweza akawa kampuni au mtu iwe/Awe na uzoefu wa utumishi kwenye nafasi za juu kwenye Saccos au taasisi nyingine za kifedha kwa muda usiopungua miaka  mitatu (3).
  2. Awe na elimu isiyopungua Shahada au Stashahada ya uhasibu.
  3. Awe na umri  usiopungua miaka 25 na usiozidi 45 kama ni kampuni iwe na uzoefu kwenye ukaguzi usiopungua miaka 3
  4. Awe na uwezo wa kufanya kazi katika usimamizi duni.
  5. Awe amesajiliwa na Bodi ya uhasibu na Ukaguzi Tanzania.
  6. Awe na ujuzi wa kutumia vyema Computer.

VIAMBATANISHO

. Wasifu wa Muombaji/ profile ya kampuni

.Nakala za vyeti vya taaluma/cheti cha usajili cha kampuni/ubia

 Nakala ya cheti cha kuzaliwa/cheti cha usajili cha kampuni/ubia

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Maombi yote kwa nafasi tajwa hapo juu yatumwe kwa barua pepe ya saccos@jatu.co.tz

Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 20/04/2020 saa kumi na moja jioni.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA BODI YA UONGOZI WA JATU SACCOS LTD

Download PDF ya hili tangazo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s