JATU TALK NI NINI? KAA TAYARI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Vijana wengi wamekua wakibuni mawazo mbalimbali ambayo yanalenga kufungua fursa za uwekezaji ila wamekua wakikutana na changamoto mbalimbali hasa kukosa mitaji na kutokua na njia sahihi za kupata wawezeshaji ili kuyafanya mawazo yao kuzalisha fursa za kiuchumi na hatimae kuchochea kuanzishwa kwa makampuni imara. JATU Talk ni jukwaa la fursa ambalo linaunganisha wadau mbalimbali wa uwekezaji kwenye fursa za kilimo, viwanda, mikopo na masoko kisha kuwawezesha kuanzisha mada na mijadala ambayo italenga kukuza mawazo ya kibunifu na kuyawezesha kupata mitaji ili waweze kufungua makampuni. JATU Talk itawawezesha wadau kusajiri kampuni au mada ambayo itawakutanisha wabunifu wa mawazo na wawekezaji ambao watawawezesha kifedha ili mawazo hayo yafanyiwe utekelezaji huku mchakato mzima ukiratibiwa na JATU.

JATU Talk imelenga kupunguza usumbufu ambao wabunifu mbalimbali wamekua wakiupata wanapohitaji kuwezeshwa mawazo yao ili kutoa fursa za kiuchumi, pia kufungua milango kwa wadau ambao wanatafuta fursa za kuwekeza kwenye mawazo ya kibunifu ila wanakosa njia sahihi ya kuwafikia. Kupitia JATU Talk tutaweza kutuma picha, video, document na ujumbe kwa kuchangia mada kutokana na wazo husika, wawekezaji pia wataweza kujiunga na wazo lolote ambalo wamependezwa nalo na kujadiliana na wabunifu wa wazo hilo ili kuliwezesha lifanikiwe.

JATU Talk itakua kwenye mfumo wa application yaani JATU Talk App ambayo itapatikana kwenye playstore kwa watumiaji wa android au appstore kwa watumiaji wa iphone. Kuanzishwa kwa mfumo huu ni moja ya malengo ya JATU kuwawezesha vijana kupata mitaji kutokana na mawazo yao ya kibunifu ili waweze kuzalisha fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kwenye kutokomeza umasikini. JATU inaamini kwenye umoja na ubunifu kama moja ya misingi ambayo itatuwezesha kupambana na janga la umasikini na kuiwezesha nchi yetu kuinuka kiuchumi na kutimiza adhma ya serikali ya Tanzania ya viwanda.

“JATU – Jenga Afya Tokomeza Umasikini”

2 thoughts on “JATU TALK NI NINI? KAA TAYARI, ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s