SAFARI YA KILINDI IMEWADIA, UPO TAYARI? ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

Habari,

Baada ya ziara ya kutembelea mashamba ya wanajatu Kiteto sasa wakati umewadia wa kwenda kutembelea mashamba yetu na kufungua kituo cha kuchakata maharage Kilindi, Tanga. Mradi wa kilimo cha maharage ulioanzishwa rasmi mnamo mwaka 2018 umekua kati ya miradi pendwa kwa wanachama wa JATU kutokana na msimu wake wa kilimo kuwa na muda mfupi yaani miezi mitatu hadi minne huku ukiongoza kwa faida inayopatikana baada ya mauzo ya mavuno ya mazao yake yaani wastani wa faida ya takribani millioni mbili kwa ekari moja.

Mradi huu ni kati ya miradi ya kilimo ya kimkakati ya JATU ambayo imelenga kuongeza kipato cha wanachama huku tukipata bidhaa ya maharage ambayo ni moja ya mboga kuu kwa watanzania wengi hivyo kuwa sehemu ya mazao muhimu kwenye kutimiza dhima ya JATU ya kujenga afya na kutokomeza umasikini.

JATU inakuletea safari hii ya Kilindi ikiwa na lengo kwa wanachama wanaoshiriki kwenye mradi wa kilimo cha maharage na wadau wengine wa kilimo kwenda kujionea na kufahamu hatua iliofikiwa kwenye maendeleo ya kilimo cha maharage na pia ikiambatana na ufunguzi rasmi wa kituo cha JATU kinachozalisha bidhaa ya maharage ambacho kimekamilika na kuanza kutumika tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Kumbuka safari hii haijalenga wanachama wa JATU pekee bali mdau yoyote wa kilimo anaweza kushiriki ili kuwa sehemu ya mabalozi wa JATU na miradi yake. Kilimo cha JATU ni kilimo cha kisasa ambacho kimeboreshwa na kusimamiwa kitaalamu huku wanachama wakiendelea na shughuli zingine za kiuchumi pasipo kuathiri kazi zao na kufadhiliwa na JATU SACCOS ambapo wanachama hukopeshwa gharama za kilimo pasipo riba yoyote na baada ya mavuno JATU hununua mazao yote kutoka kwa wakulima kwa muda sahihi ambao mkulima ataamua kuuza kwa bei itayomridhisha.

“Karibu JATU tulime bila stress kisha tukutane sokoni”

2 thoughts on “SAFARI YA KILINDI IMEWADIA, UPO TAYARI? ENDELEA KUFUATILIA BLOG YETU KWA TAARIFA ZAIDI

 1. NZURRI SANA, NA MIMI NATAKA KUSHIRIKI KULIMA NA JATU BAADA YA MSIMU HUU KUISHA. MSIMU MPYA WA KULIMA MAHARAGE NA JATU UNAANZA LINI? MIMI NIKO ARUSHA

  Like

  1. Hello Kisioki,

   Maandalizi ya msimu ujao yameshaanza rasmi jitahidi ukodi mashamba yako mapema kwani yanapatikana kwenye Jatu App, changamkia fursa. Lima bila stress na JATU kwa taarifa zaidi wasiliana nasi 0658126324

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s